Msaada kitabu cha riwaya ya asali chungu

Mtanzanika

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
2,389
Reaction score
1,131


Naomba mnisaidie niweze kukipata Kitabu hiki cha riwaya ya Kiswahili kiitwacho ASALI CHUNGU kilichoandikwa na Prof. Said A. Mohamed.
Niliwahi kuwa nacho lakini nilimwazima mtu na hakunirudishia tangu mwaka 2001.
Nimejitahidi kutafuta huko madukani bila mafanikio.
 
Umenikumbusha kitabu changu cha ZAWADI YA USHINDI sijui nimempa nani?
 
Ana sababu maalum za kukitafuta hicho...!

nimefurahishwa sana kwa kunijibia hivi....Ndugu Omonto wa-hene anapaswa kutambua kuwa Maudhui kufanana ni jambo jingine kabisa katika suala zima la fasihi simulizi.
 

Hiki kitabu ninacho ila nilikipatia Kenya. Kwa hapa Tanzania nilizunguka zunguka maduka ya vitabu japo sio Tanzania nzima nilikikosa. Sasa sijui nakusaidiaje
 
Huwa mara nyingi najiuliza ila sijaelewa. Ukienda Kenya vitabu vya fasihi hata na isimu tena vya waandishi wa Tanzania vipo kule ndo vinapatikana. Lkn kwa hapa Tanzania ambapo waandishi wenyewe ndo walipotokea havipatikani kiurahisi.
 
Hiki kitabu ninacho ila nilikipatia Kenya. Kwa hapa Tanzania nilizunguka zunguka maduka ya vitabu japo sio Tanzania nzima nilikikosa. Sasa sijui nakusaidiaje

Naomba tufanye mawasiliano tu mkuu, nitakutembelea PM ili tuone namna ya kusaidiana. Nakushukuru sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…