squirtinator
JF-Expert Member
- Sep 20, 2015
- 2,765
- 4,182
Habari zenu wanajukwaa.
Niende kwenye mada moja kwa moja. Mimi nina mwili wa wastani, sio bonge wala sio kimbaumbau. Ila nina kitambi fulani hivi, sio kikubwa sana ila kinanikera sana kuwa nacho. Sikitaki kabisa.
Hivyo mwaka huu nilikusudia kupambana nacho na kweli nimejipa muda karibu kwa wiki mara tatu mida ya jioni. Ninakimbia kilometa takribani nne ndani ya muda fulani, muda mfupi niwezao na huwa najaribu raundi ijayo nivunje rekodi yangu ya mara ya mwisho. Huwa natokwa na kasho jingi sana sababu ya mwili kuchoma mafuta. Nikitoka hapo naruka kamba. Na pia mlo wangu nimebadili toka mwaka umeanza. Nakunywa juisi ya matunda nimetengeneza hom na bites chache. Mchana mara nyingi napo nakunywa juice tu. Sipati njaa hivyo niko fresh tu na hizo juice. Pia nakunywa maji kwa siku lita si chini ya 2 mpaka 3, sinywi maji baridi.
Cha ajabu, mwili unapungua, na nafurahi ila kitambi naona hakipungui. Ni njia gani sahihi ya kupunguza kitambi bila midawa? Wazoefu naombeni msaada. Ni miezi 2 sasa ila ktk tumbo sioni mabadiliko.
Nimeamini kutoa kitambi sio kazi ya mchezo mchezo.