Msaada,kitovu kumdondokea mtoto mchanga

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
2,366
Reaction score
828
Mtoto wa kiume akikatika kitovu,na kikadondokea katika sehemu zake za siri,anaathirika?nasikia anakuwa si rijali akuwapo,je kunaukweli?
 
Mtoto kapelekwa hospitali na mdingi wake, docta akawa anamuandikia dawa, baba yake
akatoka nje kuongea na simu. Mtoto akamuinamia daktari akamwambia kwa sauti ya chini
chini, 'Dokta kwenye dozi andika Fanta Baridi,chips na kuku kila siku kwa siku 30,kutwa
mara tatu'
 
bujibuji acha masihara,,
 
Tulikuwa tunajadili wanasema mtoto mchanga wa kiume akidondokewa na kitovu sehemu zake za kiume anakuwa towashi,je kuna uhusiano gani na nguvu za kiume na kudöndokewa na kitovu?
 
Du lisemwalo lipo ni makabila mengi yanaamini hivyo ila sijapeleleza hiyo ki2 ila.kisayansi hakuna.na piya kuna mambo mengi kisayansi hakuna ila ukipuuza huwa yanatokea
 
Du lisemwalo lipo ni makabila mengi yanaamini hivyo ila sijapeleleza hiyo ki2 ila.kisayansi hakuna.na piya kuna mambo mengi kisayansi hakuna ila ukipuuza huwa yanatokea

nimeipenda hii mkuu
 
Siyo kweli !
Ni wakunga waliwaaminisha hivyo watu ili wawe makini kutunza kitovu.
Otherwise siyo kweli
 
na je kitovu kikiangukia sehemu za siri za mtoto wa kike anakuwaje?
 
Siyo kweli !
Ni wakunga waliwaaminisha hivyo watu ili wawe makini kutunza kitovu.
Otherwise siyo kweli

watu wa zamani walikuwa wanatumia vitisho ili kufanya mambo yaende vizuri. Mfano walikuwa wakikataza kukata miti sehemu zenye chemichemi kwa kisingizio ni eneo la matambiko hivyo utakufa. Walikuwa wakifanya hivyo kwa kujua/kutojua kwamba ukataji miti husababisha maji kukauka. Zilipokuja dini za wazungu wakawaambia watu wakate tu miti hamna shida. Watu wakavamia vyanzo vya maji na kumekuwa na ukame sehemu nyingi. Ni sawa na hii walitaka wamama kuwa makini na watoto wao kwani kuwa na mtoto asiye riziki ni stigma.
 
sijiliza maneno mbofu mbofu ya marehemu mr ebbo
 
Lisemwalo lipo ndugu zangu, nani yupo tayari kumfanyia majaribio mwanae? Ni bora kuamini hata kama ni imani potofu kuliko kuja kujuta baadae.
 
Jamani binafsi sijataka kuijaribu hii ingawa nimelea vidume vitupu. ila huwa wanasema na kakuwa kuijaribu ikawa kweli itakuwa ni hasara kwako basi ni bora usimjaribu.

lkn jambo ambalo ni la ajabu sana huwaga kiovu mara zote kinadondoka pembeni hata kama mtoto yuko uchi hakimdondokei tupuni sijajua kwann iko hivyo. lakin sasa ukimvesha sana manguo ndo uwa kinadondokea mbeleni
 

Teacher nipe somo hapo!Ikiwa amevaa nguo halafu kikaangukia maeneo hayo juu ya nguo inakuwaje?
 
Teacher nipe somo hapo!Ikiwa amevaa nguo halafu kikaangukia maeneo hayo juu ya nguo inakuwaje?

hkuna kitu bana shida huwawanasema ni kikimgusa utupu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…