Habari za asubuhi wadau wa mchezo, nina imani mupo salama. Naomba kuuliza kwa wale wataalam waku-edit, mimi nipo kwenye group fulani hivi la kubeti lakini huwa nakua na wasi wasi na huyu jamaa, maana mikeka yake anayoweka ni %100 ina shinda. Na mikeka yake anauza mkeka mmoja shilingi laki moja. Naomba niweke baadhi ya mkeka mniambie, je kweli ni halali au anafanya ku-editi? Maana siku hizi Mambo yamekua mengi; matapeli wako kila kona na njia za utapeli ni nyingi. Kwa anayeweza kuzichunguza hizi tafadhali.
Hiyo ni michezo ya kubahatisha huwezi sema kila siku mikeka inashinda labda kama umekuja kutangaza biashara kweli ila sidhani.atafute pesa aweke yeye kama zinashinda kweli
Mimi Naomba niwa hakikishie Mimi nimekua Niki angalia tuu anavyo tupia mkeka na KESHO yake anakuja na maneno ya shombo ya kusema toa Pesa upate Pesa. Ukweli ni kwamba lengo langu nikujua kama nilivyo eleza hapo juu. Mimi wala sitafuti biashara yoyote Ile.
Hao jamaa wako vizuri sana kwenye ku edit, hao walioleta huo mchezo ni wakenya, haiingii akilini niwe na odds za uhakika 100 kila siku, inamaana nikiweka elf 50 nakula 5M, hata nikiamua kucheza mara 3 kwa wiki ni 15M sasa 15M kwa wiki huo muda wa kufanya umachinga kwenye mitandao nitapata wapi?
Jamaa wangu achana na hizo mambo ya kununua tips. Bashiri mwenyewe wengi wana edit wawatumie wengine kama fursa sasa hiyo laki moja anataka ya nini si aongeze timu apate hela nyingi zaidi.