Babarita
JF-Expert Member
- Dec 14, 2011
- 386
- 126
Kwa taarifa nilizopata kuna jamaa wanajiita Amana Global wapo maeneo ya makumbusho sokoni wana kiofisi ndani ya soko.Sasa kuna utapeli wanawafanyie vijana wetu wanaosoma chuo,hasa ardhi na udsm.Hawa jamaa walitoa form za scholarship eti wamepata wadhamini toka uholanzi na marekani wanaitaji kusaidia wanafunzi angalau 500,kutoka vyuo hivyo viwili.Kutokana na maisha magumu ya chuo na wengine kutokua na mkopo wanachuo wakahamasika kujaza izo form na kuzirudisha.Feedback zikaja wamepata karibu wanachuo 450 na wakaambiwa waandae bajeti ya kila semista na wapeleke akaunti namba za benki,wakafanya kama ilivyo takiwa.Utata ulianza siku wanapeleka akaunti namba wakaambiwa wachangie mia 200@mwanachuo kwa ajili ya photocopy,haikuishia hapo baada ya kukabidhi akaunti namba wakapewa form inayotoa maelekezo ya kuchangia mfuko wa project ambayo ni 50000@mwanachuo ila walisema huo mchango utalipwa pale unapopewa ela yako,na wakawaambia watapigiwa simu kupewa taarifa kuhusu pesa zao.Ni muda sasa takribani miezi 3 tangu waseme watatoa ela lakini mpaka sasa hivi wako kimya na hamna taarifa yoyote na namba yao ya simu 0764491494 haipatikani tena..Sasa naomba kujua kama hawa jamaa walitumia majina na detail za wanafunzi kujipatia mradi wa kuwanufaisha wao au ni wachumia tumbo.NA NI HATUA GANI ZA KISHERIA ZA KUWACHUKULIA KWA KUWAHADAA WANAFUNZI KWA KUTUMIA DETAIL ZAO KUJINUFAISHA NA KUWAPOTEZEA MUDA WAO.