Msaada kuhusu biashara hii ya Suzuki Carry

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
Habari wana JF,

Kupitia jukwaa hili miaka miwili iliyopita nilipata mwongozo wa jinsi ya kuanzisha ujasiriamali kwa kupitia magari ya Suzuki Carry .Huu ndio ulikuwa mwongozo niliowaomba

Naomba mwongozo: Nina Suzuki Carry, nataka kumpa Dereva ambaye atakuwa akiniletea malipo kwa wiki

Kwa kupitia miongozo ya wadau nimeweza kuanza na Suzuki Carry mbili na mambo yanaenda vizuri (Mungu anasaidia).

Vuguvugu la biashara linaloendelea kwa sasa haba nchini linawafanya vijana (madereva) kupambamba sana ili kupata hesabu. Kutokana na changamoto tajwa hapo juu nimewaza kujaribu Lock-in strategy (kuingia ubia na wenye maduka: wholesalers ) ili kwa kutumia platform muafaka niwe nasambaza bidhaa zao kwa wauzaji wa rejareja (Retailers) kwa makubaliano maalum. Zaidi ya hapo nawaza kuanza kutafuta wateja mimi mwenyewe kupitia Social media kama hapa JF.

Naomba mawazo yenu ya kuunga mkono au kupinga mawazo yangu ili wengi tunufaike (wenye magari wa leo na wenye magari wa kesho)

Nawakilisha
 
Iwapo hapa JF kuna mtu anaweza kunipatia connection au anaweza kufanya biashara na mimi; anaweza kuni PM ili tuongee biashara.
 
Habari wana JF,

Kupitia jukwaa hili miaka miwili iliyopita nilipata mwongozo wa jinsi ya kuanzisha ujasiriamali kwa kupitia magari ya Suzuki Carry .Huu ndio ulikuwa mwongozo niliowaomba

Naomba mwongozo: Nina Suzuki Carry, nataka kumpa Dereva ambaye atakuwa akiniletea malipo kwa wiki

Kwa kupitia miongozo ya wadau nimeweza kuanza na Suzuki Carry mbili na mambo yanaenda vizuri (Mungu anasaidia).

Vuguvugu la biashara linaloendelea kwa sasa haba nchini linawafanya vijana (madereva) kupambamba sana ili kupata hesabu. Kutokana na changamoto tajwa hapo juu nimewaza kujaribu Lock-in strategy (kuingia ubia na wenye maduka: wholesalers ) ili kwa kutumia platform muafaka niwe nasambaza bidhaa zao kwa wauzaji wa rejareja (Retailers) kwa makubaliano maalum. Zaidi ya hapo nawaza kuanza kutafuta wateja mimi mwenyewe kupitia Social media kama hapa JF.

Naomba mawazo yenu ya kuunga mkono au kupinga mawazo yangu ili wengi tunufaike (wenye magari wa leo na wenye magari wa kesho)

Nawakilisha
Mawazo mazuri sana, naamin wenye uelewa wa biashara ya ubia / distribution wanaweza kukusaidia zaidi.
 
Ingekuwa vyema kama ungainisha rateskwa siku au kwa mwezi kwa hizo carry zako. Weka terms wazi, kwamba utasambaza bidhaa unazopewa kwa bei ya jumla, wewe uuze kwa faida au utakuwa msambazaji tu? Ukiwa msambazaji tu, gharama zako zitakuwaje? Mafuta ataweka nani? Dereva atakuwa wa nani?
 
Nashukuru kwa mawazo yenu mazuri sana.Kimsingi Mimi nitafanya kazi ya usambazi tu, madereva Ni wangu, gharama zote za Magari Ni zangu.Ninachotaka kufanya Ni kutengeneza JIT (just in Time) Service ambayo itakuwa WIN WIN kwa pande tatu (Wholesaler, Distributor na Retailer) siwezi kuweka kila kitu hapa (Strategic Information); nitumiwe tu PM halafu tutaongea zaidi. Karibuni
 
Umesomeka mkuu, yani hapo mengine ni wadau kukucheki personally.
Nadhani hapo unaweza sambaza bidhaa za zaidi ya mtu mmoja, which becomes more profitable.

Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua. All the best brother.
 
Mimi Nina Suzuki Carry nauza, kwa atakaehitaji ni 6 million. Ina vibari vyote
 
Kama MTU hana haraka sana Ni aheri kuagiza Suzuki Carry kuliko kununua kutoka kwa MTU.Kwa sasa katika soko (Tradecarview au Beforward) waweza kupata gari kwa alau Dolla 1400- 1600 na kodi ya TRA pamoja na Clearing Ni kama Tshs 4600000 mpaka 5000000 (Inategemeana na mwaka wa gari) ambapo utabakiwa na Bima ya gari pamoja na kodi ya mapato (318000 kwa mwaka). Ahsante
 
Back
Top Bottom