Msaada: kuhusu Fao la Uzazi

Mazaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2015
Posts
859
Reaction score
761
Habari wana jamvi, naomba msaada kuhusu Fao la uzazi kwa akina mama.
Mimi mke wangu amejiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF, mfuko huu umekuwa na utaratibu wa kutoa Fao la uzazi kwa wanachama wake wa kike pindi wanapojifungua na kukidhi vigezo vya Fao la uzazi vilivyowekwa.

Mapema mwezi huu mke wangu alifanikiwa kujifungua, na kwa kutambua kuwa anakidhi vigezo vya kupata Fao hili, niliamua kwenda Ofisi za PSPF Mwanza kwa ajili ya kumchukulia fomu ya maombi ya Fao la uzazi. Mara baada ya kufika ofisi husika majibu niliyopewa ndiyo yamenifanya nije hapa kuulizia.

Nilijibiwa kuwa PSPF wamepokea maelekezo/ waraka kutoka kwa Director General wao kuwa kuanzia sasa(since August 1) wamesitisha kutoa fomu za madai ya Fao hilo hadi pale maelekezo mengine yatakapotolewa.

Ikumbukwe kuwa ombi la Fao hili hudaiwa ndani ya miezi mitatu tangu kwa mdai kujifungua, nilijaribu kuwaomba wanipe uthibitisho wa kwamba nilifika ofisini kwao kuchukua fomu hizi lakini sikufanikiwa kwa sababu ya maelekezo kutoka kwa DG wao, hili nalo nilikataliwa.

Kwa ufahamu wangu (naweza kurekebishwa) Fao la uzazi bado linatambuliwa hata kwa sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii ( Baada ya kuunganishwa), sasa ni kwanini wametoa maelekezo haya bila hata kujulisha umma wa Mtanzania na bila hata ya kutoa mbadala wa nini wadai hawa wafanye ili kuja kupata haki yao hata hapo baadaye?


Kufuatia hali hii wadau mnatoa ushauri gani? Au kuna mwenye uelewa mwingine juu ya hili?
 
FAO limeenda kuendesha uchaguzi Monduli na Ukonga
 
Yan kwakweli Mungu atusaidie sana. Hii nchi imefika mahala inaumiza sana mioyo ukiifikiria, mtu unafanya kazi kwa tabu halafu unastaafu tena unateseka na visent vyako halafu tunajisifu kuwa tunajali wanyonge kweli? Hebu Raisi wa wanyonge aliangalie hili kwa jicho la pembeni, Yan kuna rafiki yangu kajifungua kafatilia fao la uzazi wanamwambia bado kanuni mpya hazijatoka sasa km walikuwa hawajajipanga na kuandaa makanuni mapema kwann waliunganisha mifuko haraka, Kuna siri gani iliyojificha? Ee Mungu tutie nguvu sana sana
 
 
Write your reply...Mi pia nilimpeleka wife ofisi za iringa nikambiwa tu kuhusu huo utaratibu sasa cjajua raha ya mufuko
huu
 
Mpaka Afike miaka 50 ndiyo tutampatia Fao lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…