Msaada Kuhusu Gari Hii

SaaMbovu

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
6,027
Reaction score
5,344
Kuna gari ipo Sokoni ni Mazda Premacy na ipo hapa Tanzania, Dar. Gari hii inamilikiwa na Afisa mmoja wa Ubalozi na plate namba yake ni ya kibalozi. Kwahiyo kama nahitaji kununua lazima niifanyie usajili pamoja na ushuru kama nilivyoambiwa na wadau wengine nje ya JF. Bei anayo niuzia ni US $3000 ambayo ni zaidi ya Tsh 4.8m.
Year: 2001
Millage: 81300
Cc:1600

Msaada
1.Je? Nikisajili pamoja na ushuru itakuwa jumla TSh. ngapi?
2. Mazda ni imara? pia upatikanaji wa spare ukoje?

Sababu ya kuuzwa ni anataka aondoke kwenda nchini kwakwe muda wake wa kufanya kazi hapa TZ umekaribia kwisha.
Msaada tafadhali nimeipenda hiyo gari.




 
magari yte imara ila ni utumiaji tu....wasi wasi wngu kwenye spare tu hapo
 
kaka kuliko uchukue MAZDA iliyotumika Tanzania, hapo haijalipiwa kodi, bora uagize kupitia BE FORWARD tena wana ofa mpaka 90% inaenda mpaka tarehe 20/03/2014. Mimi nimeagiza NISSAN X-TRAIL kwa 1,715 (CIF) najua hapo niandae kama 1,500 mpaka 2000 USD kuigomboa hapa Dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…