Jamani naomba msaada kuhusu google Chrome nataka kubadilisha Lugha kutoka KISWAHILI kwenda kiingereza. Nimejaribu kutumia ikiwa na kiswahili ila imenishinda. Naomba mniambie niende wapi ama nifanye nini ili niitoe kutoka kiswahili niipeleke kwenye Kiingereza.
Ni kwamba hicho kivinjari Google Chrome umekisanikisha kikiwa katika lugha ya Kiswahili au unataka badili ule ukurasamaskani ambao kwa kawaida ni Google.co.tz ambayo ipo katika lugha ya Kiswahili? Naomba ufafanuzi, msaada u karibu; vinginevyo napata shida kuelewa!