Msaada kuhusu hatati

Msaada kuhusu hatati

Mike 1234

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2009
Posts
1,633
Reaction score
155
Nina mpango wa kuchukua hati ya nyumba yangu,sasa mke wangu anataka tuandikishe majina yetu wawili ili isomeke wamiliki ni familia,sasa nauliza je ikitokea mkaachana hatuombei ila imetokea kisheria itakuwaje?je nitakuwa nimefanya kosa kumshirikisha kwenye hati? kwa wenye uzoefu na wanasheria naomba msaada nisije juta baadaye,
 
Mwanamke/mwanaume sio ndugu yako, leo mpo mapenzi moto moto lakini inawezekana, narudia inawezekana mwisho wa siku mkawa chui na paka- kama lengo ni kujihakikishia usalama wa baadaye kwako na kwake ni bora mkaandikisha majina ya watoto.
 
Umesema nyumba "yangu" - hivyo haiyumkini hati iwe kwa jina lako.

Ungesema nyumba yetu bila shaka mngekuwa mmeipata kwa juhudi ya pamoja na usingepata shida ya kuiandikisha jointly.
 
Mweleweshe kwa upendo tu kwamba hiyo nyumba kwa vile aliikuta asiitamani. Mushauriane na kutafuta uwezo wa kujenga nyumba ya pamoja na hiyo hutakuwa na haki ya kutokumshirikisha.

Lakini hapo upendo wenu utakapofikia kiwango cha juu kabisa (Inshallah) jambo hilo halitawaletea shida. Mtaaminiana bila shida.
 
kwani una watoto uandikishe wao iliwai kutokea moja walifanya hivyo ila huyu aliandika la mke kisha linamalizia la mume baada ya miaka mke akamchoka mume alichofanya alimfukuza mume toka kwenye nyumba yangu kamtolea vitu mume akamuliza nyumba yako au yangu mke anamwambia yangu anamwonyesha hati.
mume akamwambia mbona hii ni nyumba ni ya binti yetu mkubwa na siyo ww mm niliandika jina la binti yangu na sio ww mama aliishiwa nguvu
 
una haki zote za kuiandikisha kwa jina lako, kwa ushauri ni vizuri ukiiandikisha kwa jina lako au la mtoto wenu
 
Back
Top Bottom