Kuna kitu kinanitatiza kidogo kuhusu kidole kuvimba maarufu kama mdudu.
1. Je uvimbe wa kidole kutokana na mdudu unasababishwa na nini hasa?
2. Ni nini tiba mbadala ya kidole kilichovimba kwa mdudu ukiacha ya kwenda kupasuliwa hospitalini?
Nimeuliza haya maswali nipate kujua mana nimeshuhudia watu wengi sana wanaosumbuliwa na hawa wadudu hadi kupelekea kupata vilema vya vidole pindi wapasuapo mahospitalini.
Naomba tuelimishane naamini utakua msaada kwa wengine pia.