Habari Wadau!
Naomba msaada kujua ni sheria ipi inayo weka kikomo cha uwezo wa kukopa kwa mwajiriwa. Najaribu kuomba mkopo kibaruani kwangu nitatulie shida zangu kadhaa, ila wananiambia siruhusiwi kukopa kiasi kwamba makato yakaondoka na zaidi ya 2/3 ya mshahara, wakati mimi nataka kulipa ndani ya muda mfupi ili niweze endelea na michakato mingine. Badala wanijulishe hiyo sheria, wao wanang'ang'ana nitaishije nitaishije, jambo ambalo haliwahusu!
Natanguliza Shukrani zangu za dhati mbeleni.