Msaada kuhusu kilimo cha mahindi

GM98

Member
Joined
Dec 9, 2022
Posts
21
Reaction score
12
Habari wakuu, me ni mkulima mchanga ndo nimeanza kilimo, nina swali, hivi kuna dawa ya kuzuia mimea ya mahindi yasiliwe na wadudu yakiwa shamba au nisubir kama nitaona wadudu ndo nipulize dawa!?
 
Habari wakuu, me ni mkulima mchanga ndo nimeanza kilimo, nina swali, hivi kuna dawa ya kuzuia mahindi yasiliwe na wadudu au nisubir kama nitaona wadudu ndo nipulize dawa!?
Mbona swali tata maindi baada ya kuvuna au mmea ukiwa bado unaota
 
mmea ukiwa unaota kiongozi
Wadudu hatari Kwa mahindi ni lava ambao badae hugeuka vipepeo na wakikuwa vizuri wanataga mayai na kuendeleza tatizo
-lava Hawa wamegawanyika Kuna lava kama weupe hivi (stalk borers), wengine wanakuwa na rangi kama ya pink hivi(pink stalk borers) na wengine ni wale wanamadoa meusi au kijani hv(fall army worms au viwavi jeshi)
  • udhibiti wa Hawa wadudu ni muhimu zaidi ufanyike hatua za mwanzo yaani kila mwezi tangu mahindi kuota Hadi yanapokaribia kuchanua
  • Kuna baadhi ya dawa ambazo ni nzuri zaidi katika kudhibiti wadudu Hawa shambani kwako kama spidex( viwavi jeshi), snowmectin, dudu acelamectin, duduba, na karate ( Kwa wengine wote waliobakia).

[emoji95]Muhimu zaidi, usisubiri kuonana wadudu shambani ndo uanze udhibiti, fanya mapema Kwa usalama wa mazao yako.
[emoji120][emoji120]Kila la heri mkulima
 
Angalia picha za Hawa wadudu apa chiniView attachment 2812786View attachment 2812785
 

Asante, ubarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…