Msaada kuhusu ku-risit O level

Msaada kuhusu ku-risit O level

The Intelligent

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2013
Posts
2,459
Reaction score
824
Habari wana-education kuna kijana ameniomba nimpe msaada wa kumwezesha kurudia mtihani wake wa o level baada ya kupata matokeo yasiyomridhisha, hivyo nauliza kama mpaka sasa utaratibu wa kujiunga necta upo au amechelewa? kama upo je gharama za kujiunga bei gani? na vituo je vya kufanyia mtihani navyo vinapatikana? bei yake je?
Shukrani wakuu.
 
nenda kwenye website ya necta na wewe acha uvivu.
 
clip_image002.gif

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

TANGAZO
Kaimu Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) mwezi Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kwa malipo ya ada ya kawaida (Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT ) kimeongezwa kutoka tarehe 28 Februari, 2014 hadi tarehe 31 Machi, 2014. Watahiniwa watakaojisajili kuanzia tarehe 1 Aprili, 2014 hadi tarehe 30 Aprili, 2014 watatakiwa kulipa ada ya kawaida pamoja na faini mpaka usajili utakapofungwa rasmi tarehe 30 Aprili, 2014.
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.

Imetolewa na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.

siku nyingine uwe unatafuta mwenyewe.....
 
Hayo maelezo nnayoyahitaji mbona sijayaona kwenye website yao?
nimeshakuwekea hapo... ila ukiingia kwenye website yao angalia Tangazo CSE 2014 ... ada utalipa na adhabu so ni kama 65000 hivi na some charges za hapa na pale...muandalie dogo kama laki hivi ....
 
nimeshakuwekea hapo... ila ukiingia kwenye website yao angalia Tangazo CSE 2014 ... ada utalipa na adhabu so ni kama 65000 hivi na some charges za hapa na pale...muandalie dogo kama laki hivi ....

Asante mkuu kwa msaada wako.
 
nenda kwenye website ya necta na wewe acha uvivu.

mkuu je ni kweli ukilipia posta ni lazima ukamilishie internet cafe ya posta kwingine zoezi linadunda? nisaidie niokoe muda nisijiisumbue kwenda cafe za mitaani ambako ni jirani. natanguliza shukrani
 
mkuu je ni kweli ukilipia posta ni lazima ukamilishie internet cafe ya posta kwingine zoezi linadunda? nisaidie niokoe muda nisijiisumbue kwenda cafe za mitaani ambako ni jirani. natanguliza shukrani

wewe cha msingi nenda kituoni ukachukue namba ni bure pale.. alafu uende kufanya online registration uta upload picha ya dogo alafu utaenda nayo pale posta pamoja na hiyo elfu 65 unawambia unalipia necta o level.. kuna dirisha lao..... then wanakupa risiti unasubiri kuchukua namba kwenye hicho kituo ulicho omba....ucjal mkuu... watu wanafelli maisha sio mitihani..
 
Back
Top Bottom