Nataka kujifunza kwa kesi kwa ujumla wake na sio hii.
Kama mtu alikubali kwenye mkataba kuwa atalipa mshahara wa mwezi mmoja akikatiza mkataba bila ya notice, na akakatiza soon baada ya kupewa mshahara, hatua gani zitachukuliwa kwake?
Alaaaa kumbe!!
Haya bana :A S crown-2: lol
Ila sheria nyingi za kazi nizijuazo mimi ni huwa zinatoa uhuru kwa waajiri kujitungia sheria zao pia. Kwa hiyo, waajiri wengi hutumia huo mwanya pia ku-cover their you know what na mara nyingi hata kukitokea timbwili mtu utashindwa tu mahakani.
Fine prints ndo huwa mchawi!
Hapa unazungumzia mambo mengi.
Kwanza unapofanyakazi unakuwa na benefit nyingine zaidi ya mshahara mf. NSSF, Leave allowance nk
Gaijin hapa kwa mfano unazungumzia mshahara unapewa cash au bank.
Mimi kuna mtu alitoa notice ya 24hrs na kumbe anasafiri usiku kwenda UK
Nilikwenda Bank nikablock ule mshahara usitoke na ukarudi ofisini unless unambie
umepata mshahara ukaenda ukatoa pesa yote ndo ukaja ukaacha kazi but
kumbuka ukiajiriwa unakuwa umetoa details zako zote so watakufatilia tu wakupate
Nimekusoma kabisa umesema vyema huo ndo ukweli wenyewe
Unakuta mtu anasaini kwa muhindi mkataba hauna likizo allowance, nyumba, matibabu
Lakini haendi kokote waajiri wanatunga sheria zao
Nimekusoma kabisa umesema vyema huo ndo ukweli wenyewe
Unakuta mtu anasaini kwa muhindi mkataba hauna likizo allowance, nyumba, matibabu
Lakini haendi kokote waajiri wanatunga sheria zao
huo mkataba ni batili....
hapo ni rahisi kukamatwa kwenye malipo ya mafao yako tu...mwajiri akikujazia fomu za mafao yako kuna kakipengele mfano kwenye fomu za PPF utajaza mafao yapite kwa mwajiri na wanakukata juu kwa juu. kama vipi unaweza pelekwa mahakamani vile vile na mwajiri akudai mshahara wa mwezi, si umevunja makubaliano bwana.
ukimaanisha nini sasa hapa?Kalaga baho.......................
Yaani ukienda kuchukua mafao yako PPF lazima mwajiri wako "mliyekosana" ahusike?
LAZIMA atahusika tu Gee...
Nani anakujazia fomu zako za kwenda kudai mafao yako?
Ukibadili mwajiri bado mwajiri wa awali anahitajika kujaza taarifa zako za ajira na michango yako pia ili kuwezesha mwajiri mpya nae kuendelea kukuchangia.
Sasa hapo una pakukwepea one month salary in lieu of notice?
Gee hakuna jinsi nijuavyo mimi unaweza kupata mafao yako bila kupita kwa mwajiri(naweza kusahihishwa) na haijalishi mliachanaje ila hiyo inabaki kuwa haki yako tu, sasa kama una deni basi na yeye ndo mwanya wa kukukamata hapo.
Ukibadili mwajiri bado mwajiri wa awali anahitajika kujaza taarifa zako za ajira na michango yako pia ili kuwezesha mwajiri mpya nae kuendelea kukuchangia.
Sasa hapo una pakukwepea one month salary in lieu of notice?
Unaweza kujijazia lakini fomu zenyewe zilivyotengenezwa ni kwamba lazima kuna mahali kunahitaji mwakiri akuthibitishe/atie muhuri, sasa hapo bado una choice zaidi ya kurudi kwake?That don't make no sense whatsoever! Kwani wewe mwenyewe huwezi kujaza taarifa zako za ajira? Au ni kipi anachojaza mwajiri ambacho wewe huwezi kukijaza?
Wee mwenyewe mwanzo ulishasema kuna tatizo kwenye mfumo mzima, na mimi nimeongeza kuwa mwajiri kaachwa afanye hayo yote, ila najua statement ya michango yako unahaki ya kuifuatilia kwenye shirika husika.Tunaomba Mamaa wa HR aje atolee ufafanuzi hili, ikiwezekana. Manake kama hali ni hiyo ni makosa makubwa mno.
Kimsingi Mwajiri wangu anatakiwa kujua tu "account number" yangu ya Mafao ili aniingizie mafao yangu katika kipindi tulichokubaliana lakini hatakiwi kujua nina kiasi gani kwenye account hiyo wala kupata taarifa siku nikiamua kwenda kuchukua mafao yangu iwe bado naendelea na kazi kwake au nimeshaachana nae.
Vyenginevyo ni kuingilia faragha yangu.
btw: Mwajiri ajaze michango yake kwangu kwani huko kwenye Shirika la Mafao hawaweki kumbukumbu?
Unaweza kujijazia lakini fomu zenyewe zilivyotengenezwa ni kwamba lazima kuna mahali kunahitaji mwakiri akuthibitishe/atie muhuri, sasa hapo bado una choice zaidi ya kurudi kwake?
Halafu na sisi tulivowazembe, kama una sign mkataba unao bana haki zako, utakuwa na habari hata ya kuweko rekodi ya michango ya mafao yako????
Waajiriwa wengi wapo tu reluctant na wameacha kila kitu aamue na kuafanya mwajiri.
huwezi kulipwa kwa kuacha kazi na wala hutakiwi kulipa kwa kuacha kazi. Hawa waliotunga sheria hii kimsingi kama walifanya kumpendelea mwajiri vile. Hii sheria ni ya kizamani sana na inafaa kurekebishwa.........mazingira ya sasa siyo
BHT umeshawahi kwenda mahakama ya kazi??
Utashangaa mtu anaqoute mpaka sheria za kazi lakini
mwajiri anasema agreement yangu mimi na wewe ni
kama ulikuwa unajua sheria hii inasema hivi basi usingesaini
kusaini mkataba huu ina maana umekubaliana na masharti yangu na si vinginevyo
Sijakataa kuwa sheria hazipo sheria zipo sana tena ziko wazi
lakini utahangaika wewe na huo mshahara wa mwezi huku ukipoteza muda
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa. Uhusiano kati ya mwajiri na mwajiriwa ni contractual. Mahakama haitaweza kuingilia na kutengua terms za mkataba unless ziko au zilifanywa kinyume na sheria. Kwa mfano kama sheria inasema minimum annual holiday per year ni siku 28, halafu mkataba unasema ni siku 26 then hiyo term itakuwa kinyume na sheria na mahakama inayo haki ya kuingilia.
Pia mleta mada kama vile anadhani kuwa kwa vile hakusaini mkatataba basi hakuna mkataba. Mkataba unaweza uwe au usiwe wa maandishi. Provided that kuna sufficient consideration (promise ya yeye kufanya kazi na mwajiri kumlipa) then hapo kuna mkataba. Pia ikumbukwe kuwa hizo job offer letter na barua ya kudhibitishwa kazini may form part of the contract as well.
Maelezo ambayo mleta mada ameyatoa ni machache sana kuweza kumpa ushauri nasaha wa kisheria. Kunaweza kuwa na better options zaidi ya kutoa notice ya masaa 24 kama tukipata facts zaidi. Ila ushauri ambao siyo wa kisheria ni kwamba unapoacha kazi ni vizuri uache in good terms. You never know milima haikutani lakini binadamu wanakutana.
(5) Instead of giving an employee notice of termination, an employer may pay the employee the remuneration that the employee would have received if the employee had worked during the notice period.
(6) Where an employee refuses to work during the notice period,
an employer may deduct, from any money due to that employee on termination,the amount that would have been due to the employee if that employee had worked during the notice period.