Hadi hapa nimeelewa. Pointi kubwa ni kuwa mkataba si lazima uwe wa maandishi. Kwa hiyo kama sina mkataba wa maandishi bado napaswa kutoa notisi ya siku 28 au kama ni 24 hrs basi nirejeshe mshahara mmoja. Sasa sijui ni basic au net salary. Na je ikitokea nipo likizo na nataka kuacha kazi nifanyeje? Naweza nikatoa notisi ya siku 28 nikiwa likizo?
Mikataba mingi ya ajira huwa kuna term inayosema kuwa ukiacha kazi ni lazima utoe notice ya mwezi mmoja na kama ukiamua kuacha kwa muda mfupi, umlipe mwajili fedha taslimu inayolingana na mshahara wako wa mwezi mmoja. Unaweza ukatoa cash na kumlipa au unaacha mshahara wako wa mwishi ndio unakuwa malipo. Labda kama ungekuwa na mkataba wa maandishi kuingekuwa na hiyo term pia. I don't know.
Kwa vile huna huo mkataba itakuwa ni vigumu kuacha kwa kutoa notice ya masaa 24 kwa sababu sidhani kama utakuwa na mamlaka ya kisheria kufanya hivyo. Hata kama unaweza kutoa notice ya masaa 24 na kuondoka inaweza kukufanya ukose haki zako nyingine za msingi kama certificate of service, accrued annual leave, mshahara kwa kazi uliyoifanya kabla ya kuacha kazi, n.k. Kama ungekuwa na mkataba wa maandishi ungekuwa kimbilio lako. Kwa vile huna inabidi kuangalia sheria inasemaje.
Kwa mujibu wa Employment and Labour Relations Act 2004, notice ya kuacha inaweza kutolewa na upande wowote kwenye mkataba wa kazi. Lakini notice za kuacha kazi zinatofautiana. Kama notice ya kuacha kazi inatolewa mwezi wa kwanza baada tuu ya kuanza kazi, hiyo notice inabidi iwe sio chini ya siku saba.
Kama umeajiriwa on daily basis or on weekly basis, period ya notice lazima iwe siku nne. Na kama umeajiriwa on monthly basis, the period of notice "shall" be 28 days. Mkataba wa kazi unaweza kuwa na longer period lakini the agreed notice shall be of equal duration kwa mwajiri na mwajiriwa.
Sasa piga hesabu hapo. Kama the minimum period ya notice ni siku saba kama una mwezi mmoja kazini na siku nne kama umeajiriwa kwa siku au wiki, kweli kisheria unaweza kutoa notice ya masaa 24 kama umeajiriwa on monthly basis na umekuwa kazini zaidi ya mwaka? Labda inawezekana kuna sheria nyingine inayoruhusu notice ya masaa 24 lakini siko aware nayo. Wachangiaji wengine watasaidia kama ipo.
The best option for me ni kuongea na huyo mwajiriwa mpya na umweleze ukweli kuwa huwezi kutoa notice chini ya siku 28. Kwamba personally hudhani kuwa ni good practice kwa mwajiriwa kutoa notice ya masaa 24. Kwamba hata yeye kama mwajiri asingependa mwajiriwa wake amtwangie notice ya masaa 24. Ni muhimu kumaintain your self respect kwa waajiri wapya; kwamba you respect your employers whether old or new.
Ukumbuke kuwa mwajiri wa zamani anaweza kukushtaki for damages kama amepata hasara kwa wewe kuacha kazi within 24 hours kinyume na sheria au makubaliano. Kuna legal implications nyingi tuu na inabidi umtafute mtaalamu wa sheria za kazi akushauri juu ya hizo implications ili uweze ku-make an informed decision. Kuna issues pia za restraint to trade hasa kama huyo mwajiri mtarajiwa ni competitior wa mwajiri wa sasa na una secret business information ambazo unaweza kuzihamishia kwake. Ndio maana nimesema tokea mwanzo kuwa facts ulizotoa ni ndogo sana kupata ushauri.
Kuhusu kutoa notice ya 28 ukiwa likizo inategemea. Kwanza kabisa kumbuka kuwa ukishatoa notice ya siku 28 bado wewe ni mwajiriwa wa huyo mwajiri uliyempa notice. Huwezi kutoa notice ya siku 28 halafu ukajifanya uko likizo kumbe unafanya kazi na mwajiri mpya ndani ya muda wa hiyo notice. Mwajiri wa zamani akishtukikia anaweza kukushtaki for breach of contract and possibly huyo mwajiri mpya pia. Probably there may be exceptions.
Kama ningekuwa mimi nikishatoa notice ya siku 28 nitakuwa naenda kazini kama kawaida unless mwajiri aseme nisije. Hata kabla ya kutoa hiyo notice ningeongea nae informally kuhusiana na kutaka kuacha kazi. Who knows kama anakuthamini sana anaweza kukupa terms nzuri zaidi ya huko unakotaka kwenda.
Unless our relatioship have completely broken down, ningependa kamalizana nae in good terms na kuagana nae siku ya mwisho bearing in mind I might need a reference from him/her or something else in future. Afterall huwa napenda kuwatembelea my former employers and my former work colleagues to know how they are doing. It is all about maintaning friendship. That is my personal view, but you may have yours. Lakini kama nilivyosema mwanzo, milima haikutani lakini binadamu hukutana tena hapa hapa duniani.