Habarini ndugu, poleni na majukumu ya kila siku. Mimi nilikua naomba mnifahamishe vitu ambavyo mwanafunzi anatakiwa avifanye endapo amechaguliwa chuo fulani na amepata mkopo lakini hataki kusoma iyo kozi ivo anataka afanye application upya mwakani, je afanyaje ili akiapply mwakani asije akaathiri kupata mkopo upya mwakani kama ana vigezo??? ahsanteni.
Ahsante sana kaka kwa ushauri wako mzuri kabisa, nilichofanya ad sasa nimejisajili ndio ilihitaji hela lakini mkopo nilipata mkubwa km 90% ivyo baada ya kujisajili wiki iliyopita niukaandika barua ya kuhama kozi na majibu yanatoka baada ya wiki 2 apo UDSM. Sasa nimeamua nisipofanikiwa kubadili kozi ndo niache chuo nifanye application upya mwakani na niandike barua loan board km ulivoshauri, ahsante.