Simpo tu mkuu, kurudia mtihani maana yake ulishafanya na unataka kujaribu bahati yako kwa mara ya pili.
Unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye shule/kituo chochote kinachoandikisha wanafunzi wa kujitegemea/pc ili upewe namba rejea ambazo kila kituo hupewa na baraza la mitihani.
Kwa kawaida namba hizi huwa bure kwa mujibu wa baraza , lakini andaa elfu 30 mpaka 50 kwa ajili ya kuilipia kwa jina ya gharama ya kituo husika, lazima utatakiwa kulipia gharama hizi katika shule/kituo husika.
Ukipata ref namba unaekwenda nayo mara nyingi posta ya karibu wana dirisha linalohusika na ulipiaji wa mitihani kwa wanaorudia.
Gharama za hapo huwa 65 kwa maana ya mtihani elfu 50 na gharama za posta wao huchukua 15.
Posta watakachohitaji; namba yako ya mtihani uliyofanyia awali mfano s4554/6766/2017, kituo unachofanyia, sanduku lao la barua, email kama unayo na masomo unayorudia.
Ukiwapa ndani ya dakika 5 wanaingiza taarifa hizo na kukupatia karatasi yako ya usijali. Unaweza kuitoa kopi ukapeleka kwenye shule/kituo husika kwa rejea ya baadae.
Hapo unakua umemaliza jukumu lako na namba yako ya mtihani husika itatumwa kwenye kituo chako mwezi mmoja kabla ya siku ya mtihani. Utaenda kuichukua kwa mkuu wa shule/kituo katika muda huo tayari kwa kuanza mapambano mapya.
NB: wanaorudia mitihani hawana continuous assessment mana wao sio wanafunzi endelevu wa shule. Unajisome binafsi au baadhi ya shule/vituo hufundisha kwa mfumo wa tuition. Lakini hata kama utakua darassni na kufundishwa hutakua na alama endelevu, wewe unapambana na paper ya necta tu.
Faida yake, huvai uniform siku ya kwenda kwenye mtihani wa necta. Unatupia chchote kwa mujibu wa tamaduni za Mtanzania unazama mahakamani.
ANGALIZO: Katika kila mtihani kumbuka kubeba ile karatasi yako yenye namba ya mtihani utakayoipata toka kwa mkuu wa shule/kituo mana ndio kitambulisho chako.
Ingawa wasimamizi wanakua na sheet
nyininge toka necta yenye majina na picha zote za watahiniwa, ila nawe ni lazima kuwa na barua yako. Usijaribu kudanganya wana data zote za watahiniwa wa kituo husika.
Sent using
Jamii Forums mobile app