Msaada kuhusu magari ya zamani

Democrasia

Member
Joined
Feb 1, 2008
Posts
79
Reaction score
3
Wadau poleni na majukumu ya kujenga taifa hili, mimi ni mfanyabiashara wa shughulu za usafirishaji, nimekuwa kwenye biashara hii kwa takriban miaka 12 sasa, nimekuwa nikitumia Landcruser na Landrover kama vyombo vya usafiri. wiki iliyopita nilikwaruzana na mmoja wa wafanyakazi wangu ambaye ameolewa na mfanyakazi wa Mamlaka ya mapato idara ya Forodha, baada ya kukaa kwa takriban wiki mbili walikuja maofisa wa TRA idara ya forodha na kuniamuru niwapatie kadi za magari yangu na wakazichukua kwa minajili kuwa zitakuwa kwenye uchunguzi kwani hazikulipiwa kodi wakati zinaingizwa nchini na kama zililipiwa kodi nipeleke risiti husika, cha kushangaza zaidi wakaniambia kama nazitaka hizo gari nilipe kiasi cha shilingi milioni 145. ikumbukwe kuwa magari hayo nilinunua kwa watu na walichonipatia ni kadi za magari halisi tuu, wakati wanazichukua zilikuwa zimebaki siku 4 road licence iishe, na baada ya hapo nililipa kama kawaida sasa nashindwa kuelewa tatizo liko wapi.

Naomba wadau mnifafanulie
 
angalia gari kama inadaiwa kwa kutumua neno Kadiria no ya gari kwa 15341

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…