Msaada kuhusu malipo ya ada yanayolipwa na Bodi ya Mkopo (HESLB)

okyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
2,003
Reaction score
1,507
Habar zenu wanajukwaa...!

Nimekuwa nikipata mkanganyiko kidogo kuhusu swala la ada inayolipwa na bodi ya mkopo kwenye vyuo vikuu

Pale ambapo mwanafunzi anapata mkopo bodi humlipia mwanafunzi huyo pesa ya meals and accomodation na tution fee kwa ile percent ambayo mwanafunzi amepewa na bodi ya mkopo

Sasa mkanganyiko wangu mi upo sehemu moja tu kwenye swala la mwanafunzi kutakiwa kusaini ada pale ambapo bodi inakuwa imefanya malipo ya hiyo ada, imekuwa ni tabia ya vyuo kudai wanafunzi kulipia ada pale ambapo mwanafunzi hakusaini ile ada ambayo bodi ya mkopo ilimlipia

Sasa mkanganyiko unakuja hapa je kwanin vyuo hivi huwataka wanafunzi hawa kulipia tena ada kwa sababu hawakusaini

1: je ni kwel vyuo hivi hurudisha hizo ada ambazo wanafunzi hawajazisaini?

2: Na kama hawazirudishi kwanin wanadai hawa wanafunzi walipe ada tena kwa mara ya pili ingali walishapokea pesa kutoka bodi?

3: Kama pesa hizi hazirudishi vyuo huzipeleka wapi pesa hizi ambazo huwadai wanafunzi wazilipe tena?

4: Je mamlaka husika kwenye hivi vyuo haviyaoni haya?

Wanajukwaa hapa nimekwama naomba msaada maana najua wazu hapa kuna watu wanauelewa mkubwa kuhusu haya mambo ni matumaini yangu nitapata majibu yanayoridhisha.

Nimeamua kuandika uzi huu kwa sababu kuna ndugu yangu amemaliza chuo kimoja hapa nchini amekumbana na kadhia hii na alienda bodi ya mkopo akapewa statement inayoonyesha malipo yote ambayo bodi iliyafanya tangu alipo anza masomo mpaka alipomaliza.

Statement hiyo hakuna mahali ilipo onyesha kuwa bodi haijafanya malipo ya iyo ada anayodaiwa

Pia chuo kilimtaka apeleke cheque namba ambayo bodi ilifanya malipo ya iyo ada, alipoenda bodi wao walimjibu akawaambie chuo wampe cheque namba ambayo inaonyesha chuo kilirudisha iyo pesa bodi.

Wanajukwaa karibu kwa msaada
 
Chuo gani hicho? kwanini alikuwa hasaini pesa ya ada? nijibu kwanza maswali hayo.
 
Alisain ila akiwa mwaka wa kwanza hakusaini muhula wa kwanza sasa ameenda chukua cheti ndo wanamwambia alipe ada ya muhula mzima
 
Ni chuo kimoja cha serikali kipo dodoma mkuu
 
Alisain ila akiwa mwaka wa kwanza hakusaini muhula wa kwanza sasa ameenda chukua cheti ndo wanamwambia alipe ada ya muhula mzima

Inawezekana pesa haikutumwa chuoni na kama ilitumwa na hakusaini ni kosa lake afuatilie chuoni pesa itakuwepo.
 
Bodi inaonyesha walimlipia ada kabisa mana ilibidi akafuate statement makao makuu dar akapewa statement ambayo ilionyesha malipo yote ambayo bodi ilimfanyia sasa alipoenda chuo wakamwambia hakulipa ilibidi arudi tena bodi wao wakamtaka aende chuo akachukue cheque namba ambayo chuo walirudishia iyo pesa bodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…