Msaada kuhusu malipo ya siku za sikukuu

LastCall

Member
Joined
Aug 8, 2014
Posts
22
Reaction score
8
Wakuu habari zenu,
Kwa wataalam wa sheria ninapenda kujua jambo lifuatalo kwani kuna ndugu yangu amejikuta ktk mvutano na mwajiri wake ili tuone kama kuna namna anweza saidika.
Mosi ya alikuwa ni mwajiriwa kwa mkataba wa muda maalumu, ambapo katika mkataba wake kuna vipengele vinavoelezea namna ya malipo yake yatakavokuwa, kwamba atakuwa na fixed salary ambayo itajumuisha msaa ya ziada. Na kuwa kampuni itatambua uwepo wa sikukuu zisizozidi 18 kwa mwaka na endapo atafanya kazi ktk mojawapo ya siku hizo atalipwa kwa mjibu wa mkataba.

Mkataba pia unasema atakuwa na siku moja ya kupumzika kila wiki ambayo yaweza kubadilika kulingana na mahitaji ya kampuni anayoifanyia kazi. ( IKumbukwe huyu ndugu kaajiriwa na kampuni A akawa outsourced kufanya kazi kampuni B ambayo inamlipa mshahara kupitia kampuni A.

Mkataba umefika mwisho na sasa huyu ndugu anadai malipo ya kinuwa mgongo kwa mjibu wa sheria na mkataba, lakini pia malipo ya siku 31 za sikukuu alizofanya kazi. Mshahara wake Gross kwa mwezi ilikuwa ni 1,250,000/=. Mwajiri hayuko tayari kulipa hizo siku za sikukuu kwa madai kuwa kampuni ilitoa mikataba ambayo yeye anahiita (Standard contract) na kuwa kipengele hicho kinalihusu kundi jingine. Ukiangalia mkataba unasema ni kati ya X kwa maana ya mwajiriwa na Y kwa maana ya mwajiri.

Je huyu mdogo wetu hastahili kulipwa hizi siku za sikukuu pamoja na kinuwa mgongo kweli? Kama ndio kwa nini huyu mwajiri aliweka hivi vitu kwenye mkataba? Na ikiwa sheria ya kazi inatambua kuwa mkataba ni makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa.

Naomba ushauri hapa naamini wataalam wa kutafsiri sheria wapo. Ikibi nitauweka mkataba wenyewe pia ikiwa utahitajika.
Asanteni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…