Msaada kuhusu Masters ya Open University

ndugu yako

Senior Member
Joined
Mar 30, 2013
Posts
193
Reaction score
96
Habar za humu wakuu, mimi ni mwajiriwa mpya serikalini, na katika mipango yangu ya muda mrefu ni kusoma master pindi nitakapopata permanent employment.

Kwa bahati mbaya nimepangiwa mkoa ambao una chuo kikuu kimoja cha Open University, Katika uelewa wangu najua Open wana utaratibu tofauti na vyuo vingne na hta mtu mwenye Pass anaweza kusoma master na pia masters zao ni za muda mfupi tofauti na vyuo vingine.

Sasa swali langu linahusu value ya hii master kutoka Open University, je nikiamua kusoma huko hiyo master yangu itakuwa na value sawa na masters za vyuo vingine au ndo nitakuwa nasengenywa "...... atatuambia nini wakati ana masters ya Open huyo"?!

Msaada wenu wakuu tafadhal!!
 
Acha ufinyu wa mawazo Wewe...Open University Of Tanzania ni chuo cha serikali tena kikongwe kuliko vyuo kibao nchini kama UDOM, MZUMBE, SAUT, TUMAINI etc kutoa only UDSM na SUA. OUT hakichukui mabogas ka Wewe wenye Pass mark...tafuta vyuo vingine ukasome iyo Masters yako.
 
Inaonesha bado kabisa huko brainwashed kaka, dhumuni la kusoma ni kujiongezea maarifa na sio kuogopa kusengenywa na wengine.

Inasikitisha kwa msomi kama wewe kuwa na uelewa finyu wa masula ya elimu.

Pathetic!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…