Pole kwa yaliyokutokea, lakini usijali, Kisheria si kosa, isipokuwa unatakiwa kuwaandikia TRA (Regional office yako ukiwajulisha kwamba katika 'cheque' namba fulani kulifanyika makosa ya kutotofautisha kati ya VAT na Provissional Tax, bila kuwapa taarifa 'Tax Account' yako na TRA itaonyesha kodi fulani umelipa zaidi na aina fulani ya kodi unadaiwa. Kwa namna nyingine unaweza kufuatilia TRA kujua kama cheque yako uliyolipa imewekwa fungu gani, kwa mfano kama imeingizwa katika 'Provissional Tax' 3rd Instalments na amount ni zaidi ya ulichotakiwa kulipa kama instalments, basi 4th Instalments utaipunguza ili katika mwaka usiwe umelipa zaidi ya kodi uliyokadiriwa ya 'Provissional tax'. Huu ndiyo ushauri wangu kwako juu ya masuala ya kodi.