Brightman Jr
JF-Expert Member
- Mar 22, 2009
- 1,224
- 234
Crdb wana unafuu kidogo. NBC usijaribu hao ni hatari. Wana riba kubwa sana. Mfano ukikopa Tsh 1.8M utalipa Tsh 2.8M.
Muhimu zaidi unapoenda kukopa bank hasahasa personal loan uliza interest wanai-calculate au accumulate how? Mfano. Nmb wanatumia straight line methodi ambayo mteja atachajiwa kiasi sawa toka mwanzo wa mkopo hadi mwisho wa mkopo. Ukikopa 10m, ukalipa interest ya tzs 190,000. So deni litapungua kwa hizo hela, kwahiyo interest inatakiwa iwe pungufu ya ile ya mwanzo, lakini kwa njia hii ya straight line, hata kama utalipa na kubakiwa na deni la laki moja, bado utailipia ile m10 ya mwanzo tofauti na crdb ambao wanatumia reducing balance yaani unalipia unachodaiwa tu.
Muhimu soma mkataba kabla hujausign.
CRDB pia wanapiga watu penalty. Kama tarehe ya kulipia mkopo ni 25 na akaunti yako haina pesa siku hiyo, siku pesa ikiingia kwenye akaunti wao watakata pesa yao na cha juu pia.nmb wana mikopo mizuri ukijumuisha na straight line method ya installments tatizo lipo kwa kwa ma loan officers 1.wanapenda sana rushwa 2.wanamnyima mteja uhuru wa kuusoma ule mkataba na kuuelewa vizuri 3.kuwa makini na payment period unaweza omba miaka 3 wakakuwekea miaka 5 au wakakuwekea mitatu fresh bt but unakuta wanazidisha miezi kadhaa mbele baada ya mda unaotakiwa kupita.CRDB is the best bt hizo process ndio shida utafikiri unataka kukopa trilion.
Hapo ndipo nasikia mwili kusisimka ndugu yangu.
Loan processing ya nini tena wakati kuna riba riba nalipia,na hiyo insurance ya nini,kwani inarudishwa ikiwa nitarudisha kiasi chote cha mkopo?
Na vipi swali la 3,unaweza kunisaida ufafanuzi mkuu? Mshahara wangu (take home) ni laki 8 na visenti senti je kwa NMB na wezapata max mkopo wa tsh ngapi mkuu?
Samahani lakini kwa maswali mengi ndugu yangu.
Loan insurance fee hairudishwi bali inakusaidia wewe kama ukifa au ukipata matatizo mengine yatakayokufanya ushindwe kulipa, hutadaiwa.
Mh kwa mshahara huo mkuu huwezi pewa mkopo wa million 10, lazima uanzie chini ya hapo kama 2m kwanza then ukienda nao vizuri wanaenda wanaongeza