Msaada kuhusu mikopo

PRINCEd

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2015
Posts
860
Reaction score
620
Leo katika pitapita zangu nikaona tangazo la NMB kuwa kwa sasa wanatoa mkopo nafuu kwa watumishi na wamesema ni asilimia 11% pia kuzingatia 1/3 ya
mshahara.....

Maswali yangu..
1. Iyo 1/3 ya mshahara inahesabikaje? Je, ni katika basic salary au take home?

2. Mfano mtu anaepokea take home ya tsh 470'000/= baada ya makato kutoka bodi huyu 1/3 yake ni shiling ngapi??

3. Mwenye uelewa hapo hiyo riba ya 11% kwa mwaka mfano mtu uchukue milioni 10, utarejesha shilling ngapi baada ya miaka 5?

Naomba kuwasilishaaa
 
Pita hapo Benki wauulize wao utapata maelezo zaidi.. Maana Wengine mikopo hatutaki kwa sasa
 
Unashindwa kupiga mahesabu ya 11 asilimia ya 10M .

Hapo ni laki moja na ushee
 
Ni Basic,
Basic Salary /3 Jibu Utakalopata Unatoa Take Home
Kwa Hiyo Chukua Basic Gawa 3,halafu Chukua 470,000 Toa Jibu La Juu,utakayopata Wasilisiana Na Afisa Akuangalizie Kwenye System Mkopo Unaoqualify,pia Kumbuka Ukikaa Na Mkopo Mda Mrefu Riba Kubwa Ila Makato Ya Kila Mwezi Madogo,ukichukua Mkopo Wa Muda Mfupi Makato Ya Kila Mwezi Makubwa Ila Riba Ndogo
 
Ni Ngumu Kukujibu Mkopo Wa 10m kwa miaka 5,kwa take home yako mpaka uwe unafanya nmb,kila bank ina system au schedule kwa hiyo mjomba ungerudi nmb ingependeza zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…