Msaada kuhusu mimba pls

Kifai

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
816
Reaction score
173
Habari zenu wataalamu wa jukwaa hili hapa, natumaini wote mu wazima wa afya tele!!!!!!! Mai wife ana ujauzito sasa wa takribani miezi sita sasa, ila tatizo amekuwa akienda haja ndogo kila mara, yani ndani ya nusu saa anaweza kwenda hata mara tano mpk saba, cjui tatizo nini, mwenye kujua naomba ushauri pls, asanteni na mungu awabariki
 

Hilo ni tatizo na linaweza kuwa ni UTI inamsumbua!, Mpeleke hospital mapema iwezekanavyo!
 

Naunga mkono mwenye amechangia wa kwanza hiyo inaweza kuwa UTI nadhanj unaexagerate anaenda mara ngapi kwa nusu saa? Na anakojoa mkojo kiasi gani? Ukitaka kupata ushauri wa afya usifanye kama wanasiasa
Pili maelezo
Mwanamke mjamzito kupata haja ndogo mara ni kawaida kidogo kwa maana mfuko wa uzazi unakua na kujaza tumbo compression ya kibofu cha mkojo hivo kibofu hakiwezi kuhimili ujazo wa zamani

Kutokana na mabadiliko ya kihormoni katika njia ya uzazi na mkojo pia wanakua na hatari ya UTI zaidi ukilinganisha na mwenye sii mjamzito

Wanawake wajawazito pia wanaweza pata kisukari cha uzazi? Gestational diabetes utaisoma hata kwa simu yako kujielimisha kwa ufupi mama atakua anakojoa sana anakula sana na anakunywa sana

Kwa maelezo zaidi mwone dakitari ameone mkeo chonde usimtibu mwanamke mjamzito kwa ushauri wa jf..au mtandao mwingine wa kijamii hapa tunakupa maelezo ya tatizo kukujuza zaidi kulngeza uelewa wako kuhusu tatizo hivo kama kweli unampenda muwahishe kwa paramedics
 
kaka mpeleke akafanye check up kwa hospital,maana ujauzi unamambo mengi,unaweza kusauriwa na mtu humu mpe kitu flan kumbe ndo chanzo cha kuharibia kwa ujauzito,
 
ukiwa mjamzito mimba ikiwa kubwa ni kawaida kukojoa mara kwa mara,kama una wasiwasi mpeleke hospitali,ila naamini hakuna tatizo
 
Mwanamke mjamzito kukojoa mara kwa mara ni kawaida kwani tumbo la uzazi linakua limekandamiza kibofu cha mkojo na kufanya kiwango cha uhifadhi kuwa kidogo na kupelekea kukojoa mara nyingi ukizingatia wanawake wengi wajawazito wanashauriwa kunywa maji kwa wingi...ila kwa vipimo na ushauri nenda hospitali
 
Msome tena smallville halafu chukua hatua.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…