Mwaka jana niliomba chuo na nikapata. Pia niliomba mkopo ila sikupata hata asilimia 0. Kutokana na kutopata mkopo nilishindwa hata kwenda kiripoti chuoni badala yake ilinibidi kujipanga mwaka huu niende kwa kujilopia. Habari ambazo ninazipata ni kwamba mwaka jana data zinasoma kuwa nilipata mkopo kwa hiyo siwezi kupata mkopo kwa mwaka huu. Je wadau nifanye nini hapa ili niwe salama? Maana kama ni kweli nilipata mkopo alafu ukachakachuliwa si inaweza kula kwangu? Kwa sasa niko chuoni na nimekamilisha usajilo hapa UDSM.