Msaada kuhusu nywele pamoja na ngozi yangu.

Crisheb956

Member
Joined
Dec 26, 2018
Posts
21
Reaction score
13
Poleni na majukumu wapendwa.

Kama tulivyo wengi nina kipili pili balaa.nikichana nywele kichwa kina uma. Natamani sana nifuge nywele natural ila kuchana ndo mziki.....nikikaa mda mrefu bila kuchana nikija kuchana kichwa kinauma na nywele zina katika.

Naomba ushauri wa mafuta ya kulainisha nywele. Ili niweze kuchana hata zikiwa kubwa.

Kuhusu ngozi nina ngozi sensitive. Na pia mimi ni chocolate colour kuna kipindi napata pimples kuna kipindi zinapotea.

Uso wangu una mafuta. Ila nisipo paka mafuta or lotion inakua dry. Naomba msaada wa mafuta au lotion ambayo aita nichubua ila itakayo nisaidia kuondoa makovu pamoja na pimples.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa kuanzia. Tumia alovera kwa kujipaka mwilini ikiwemo na usoni na kichwani pamoja na kunywa juice yake.

Lapili pendela kula matunda ya Avacado, kwa ajili ya ngozi pamoja na kunywa maji mengi kwa siku hata lita 3 kw uchache.

Wenegine watajalizia.
 
Mi na shida kama yako mtoa Uzi, natumia mafuta ya Nazi usoni na mwilini, naogea magadi, maji nakunywa sana maana ni muhimu kwa ngozi. Usisahau kuwa unatembea na kitambaa juani kujifuta pia kunawa uso unapotoka kwenye mizunguko maana unakuwa na bacteria wengi umekutana nao.

Kuhusu nywele tumia conditional ya asali pia mafuta ya vatika au amla mazuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante Mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…