Msaada kuhusu Rais kutoshtakiwa

othuman dan fodio

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2018
Posts
6,850
Reaction score
11,033
Kuhusu Rais kutoshitakiwa, muda sio mrefu kesi aliyoifungua Edo Shaibu akisimamiwa na wakili Fatuma Karume dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli imegonga mwamba.

Moja ya kigezo cha kugonga mwamba ni kwamba maombi hayo yamekiuka kifungu cha 46(1) na (2) cha katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivyo kesi kuwa striked out.

Sasa naomba kuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwa mfano mtumishi wa umma imetokea umefukuzwa kazi kwa uonevu, kwa mujibu wa sheria zilizopo unatakiwa u exoust all local remidies nikimaanisha umalize taratibu zote za rufaa za kiutumishi kwanza ndipo kama bado hujaridhika ndipo unaenda mahakamani kuomba judicial review.

Sasa kama mnavyo fahamu mamlaka ya mwisho ya rufaa kwa watumishi huishia kwa Rais ambaye yeye ndio mwajiri Mkuu.

Je nikienda kuomba judicial review nitamuweka President kama first respondent au nikifanya hivyo nitakwenda kinyume na matakwa ya Katiba?

2. Na je kesi ikiwa strike out ndio basi tena au naweza kuja kivingine nikaifungua upya?

Karibuni wadau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…