Msaada kuhusu sheria za kazi na ajira

Akiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Posts
1,445
Reaction score
214
Msaada wana Jamvini



Mimi ni mfanyakazi wa taasisi fulani hapa Dar. niliaanza kazi tarehe 01/04/2013 mwajiri wangu hakunipa mkataba wowote wa maandishi.. lakini baada ya miezi 3 akanipandishia mshahara na mwezi wa tisa akanipandishia mshahara tena na moja kwa moja akaniingiza kwenye mfumo wa payroll , leo mwezi wa tatu 2014 nikiwa namaliza mwaka ananipa mkataba wa maandishi anataka nisaini kwamba anaanza tarehe 1/06/2013 na unaisha tarehe 31/06/2014.

nikamuuliza si inabidi nisini kuanzia siku unayonipa huu mkataba amekataa anasema mwanzo alitaka kunipa mkataba wa permanent lkn sasa hivi amebadilisha utaratibu. lkn cha kushangaza utaratibu huo anaotumia kwa mimi tu wengine wapo kazini wana miaka zaidi ya kumi na hawana mkataba.

Je naomba mnisaidie ni sahihi kuandika mkataba wa maandishi kwa kuanzia tarehe za nyuma?

Asante.
 
Mkataba unaanza siku mtakayosign mkataba tu.
Asante kwa ushauri, ni vp naweza kugomea kusaini na nikawa salama? maana nimegundua ana nia ya kunifukuza kazi na ndiyo maana analazimisha nisaini tarehe ya mwaka Jana ili mwezi wa sita mkataba uwe umekwisha .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…