Msaada kuhusu Sheria za kazi serikali mkuu.

Rwebo

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2015
Posts
1,418
Reaction score
1,820
Niliajiriwa serikalini kwa masharti ya kudumu. Nilifanya kazi kwa muda wa miaka 15 na miezi 9 niliacha kazi bila kufukuzwa na wala siku andika barua kwa Katibu mkuu wangu wa wizara. Nina vielelezo vyote kama: Placement latter, Employment latter, confirmation latter, salary slips na Kitambulisho cha kazi. Shida yangu je, naweza dai pension yangu niliokuwa nachangia kwa muda wote huo? Sababu sasa hivi nina umri wa miaka 56. Naomba msaada wenu wa kisheria.
 
Hiyo ni haki yako.
La kufanya nenda ofisi yoyote ya PSSSF ukapewe fomu ya kupeleka kwa mwajiri wako pamoja na maelekezo mengine.
 
Hiyo ni haki yako.
La kufanya nenda ofisi yoyote ya PSSSF ukapewe fomu ya kupeleka kwa mwajiri wako pamoja na maelekezo mengine.
Asante sana nashukuru
 
Huwezi kupewa pension bila kuwa na ama termination letter au retirement letter. Watajuaje kama umeacha kazi bila kithibitisho??

Kwanini uliacha kazi kienyeji?? 15 years of service tayari ulishakuwa pensionable, ulipaswa ufuate taratibu za kisheria za kuacha kazi na kisha ungeenda kwenye mfuko wako wa hifadhi ya jamii ukiwa na kibali chako cha kuacha kazi then ungepatiwa kiinua mgongo chako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…