Hello wadau nahitaji msaada wa kitaalamu zaidi kuhusu tatizo la Mwanamke kuingia Bleed mara 2 kwa mwezi, Nina mchumba ambaye ana tatizo hilo, wakati mwingine humtokea na kuingia mara 2 na wakati mwingine inakuwa mzunguko wa kawaida wa siku 30
Nahitaji kujua sababu ya tatizo hili, tiba yake na nini madhara yake! Naamini nitapata kujifunza kutoka kwenu!
Natanguliza shukrani
Mkuu hii kwa kitaalamu tunaita metrorrhagia! (Irregular menstral bleeding), hii ni dalili ambayo inaweza ikawa inasababishwa na mambo mengi kutegemea na umri wa mwanamke!
Kwanza inabidi utuambie kama anatumia dawa za uzazi wa mpango? (Contraceptive pills!), kwasababu mara nyingi wanawake wanaotumia hizi dawa hua wanapata break through bleeding ambazo hutokea katika ya siku zao za kawaida!
Pili mkuu! hii dalili inaweza ikawa ni kiashiria cha uvimbe kwenye mfuko wa kizazi sana sana (uterine fibroids) ndo hua ni common zaidi!, au pia kuna aina nyingine za uvimbe kama uterine polps, adenomyosis lakini hizi sio common sana!!
tatu mkuu! Kutegemea na umri wake hii inaweza ikawa ni kiashirio cha kansa!! Kuna endometrial carcinoma, cervical carcinoma na kadhalika! Ila hizi ni kwa wanawake ambao umri kidogo umeenda!
Na mwisho mkuu! Hili tatizo laweza likiwa limesababishwa tu na hormone imbalance!
So Kwa ushauri ! Mpeleke shemeji hospitalini akafanye kwanza ultrasound ili tujue kama kuna tatizo kwenye mfuko wa uzazi, baada ya hapo madaktari watajua cha kufanya!
Asante sana Mkuu kwa ushauri wako wa kitaalamu, nimejaribu kumuuliza kuhusu kutumia njia za uzazi wa mpango, ameniambia amewahi kutumia vidonge kwa kipindi cha miezi mitatu, vikamletea tatizo la kupitiliza siku, kutokana na maelezo yako nadhani ni sababu mojawapo.Mkuu hii kwa kitaalamu tunaita metrorrhagia! (Irregular menstral bleeding), hii ni dalili ambayo inaweza ikawa inasababishwa na mambo mengi kutegemea na umri wa mwanamke!