Kuna mzee aliniomba ushauri nimsaidie kununua hiace kupitia internet, ikapatikana kwa CIF 7310 USD. Nikamuangalizia kodi kupitia TRA calculator ambayo ilionyesha kuwa atatakiwa kulipa kodi ya TSHs 4,580,000. Gari imeshafika dar bandari TRA assessment inaonyesha anatakiwa kulipa milioni 11,350,000 kama kodi tu. hivi inakaaje wanaJF. Jana mzee amenipigia simu huku amechanganyikiwa hajui afanye nini...