Msaada kuhusu ubora wa water pumps

Samson Kasaki

Member
Joined
Jul 6, 2016
Posts
6
Reaction score
1
Wadau wangu wa ukweli mnisaidie kuhusu hizi mashine za umwagiliaji bustani:
1. Zipi zenye ubora kati ya
Honda na Kingmax?
2. Namna ya kuitambua
waterpump "original" wakati
wa kuinunua dukani
( ikiwa mpya). Naamn
mtanipa ushirikiano,
Nawasilisha mada.
 
Kwa uzoefu Wangu wakutumia machine cha muhimu nikufuata manufactural instruction. Pili narecommend honda
 
Asante! Ila kwenye manufacturer instruction utujuaje hip feki na IPI original?
 
Honda ndio mpango mzima sema bei itakua kubwa,
Nenda kwenye maduka ya wakala wao ambao ni Quality Group, ukinunua kwa duka la kawaida guarantee ya kuuziwa feki ni kubwa.

Hata Kingmax kuna nzuri ila feki nyingi. Usinunue KM ukaambiwa ni Kingmax, SIO KWELI ingawa boksi zinafanana picha.
Nunua Kingmax ambayo maandishi yamevimba/yametokeza nje au kubonyezwa kwa ndani, sio KIingmax ya Stika tu, utaliwa.
 
Angalia bei Honda original zina warantii ila bei juu
 
Asante kwa ushauri mzuri!
 
waterpump zote ni nzuri na watu wanaendeshea maisha bila shaka. Nikupe experience kidogo. nilienda kariakoo shimoni nikanunua honda yenye stika (ya mchina) nimeitumia mpaka leo hii nnaitumia Morogoro kulimia. Inachohitaji ni matunzo tuu.Nunua oil ya Bp ambayo bei yake iko juu zaidi ya oil za kupima nakuhakikishia jino moja tuu waterpump inawaka. kitu kingine bi kubadili tuu plug inapochoka na unapovuta ile kamba yake ya kuwashia jitahidi usivute mpaka mwisho la sivyo utang'oa kamba ilipofungwa kwenye mtego ni pa plastic. Kuna dogo langu moja limenunua kingmax ya mchina ina miaka zaidi ya nne sema anaitunza vizuri. Kwa maji ya Dar yenye chumvi frame yake yote imeliwa na kutu lakini jino moja tuu inawaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…