Msaada Kuhusu Ufugaji wa Kuku wa Mayai

Brown Mduma

Senior Member
Joined
Sep 29, 2020
Posts
180
Reaction score
284
Wakuu mwenye kujua changamoto za ufugaji wa kuku wa Mayai na namna kuzikwepa anipe muongozo kidogo kwasababu kuna jamaa mmoja alinisimulia juu juu tu kuhusu ufugaji huo akidai nikiwa na kuku 300 niweza pata hadi trey 18 kwa siku kuku wa kishaanza kutaga sasa kwa upande wangu nimeona ni fursa nzur kama naweza nikakomaa nayo vizur inaweza kunitoa kimaisha maana mtaani pagumu sana wakuu.

Nia Yangu ni kwamba ni pangishe chumba kikubwa ambacho hata kisipokuwa na umeme sawa lkn niwe nawafuga kwenye chumba cha 10×10 at least au kinachozidi hicho ambacho kipo uswazi kodi isiyozidi 30 kwa mwez. Na vile ningependa kujua ninaponunua vifaranga(mbegu) vitachukua mda gani kufika kuanza kutaga.

Ambae anaexperience na ufagaji huu naomba usisite kunipa muongozo mzur ili niweze kuanza niwe nishajua nini chakufanya
 
Hongera kwa wazo zuri la kufuga mkuu, Ila hebu nikupe moyo wa kuanza hata kwa kuku wachache kwanza Kama hujawahi kufuga kabisa(kisasa). Au Kama utakomaa kuanza na wengi basi jitahidi sana kuwa karibu na wataalam wa mifugo au mtu mzoefu (aliyefuga na akafanikiwa).

Ila naomba ujue vitu muhimu vifuatavyo:
1. Ukiwa na kuku wa kutaga 300 tegemea kupata mayai 240 mpaka 270 Kama umewahudumia vizuri kuanzia wakiwa vifaranga.

2. Kuanzia kifaranga mpaka afikie hatua ya kutaga huwa ni miezi 5 mpaka 6 kutegemea na aina ya kuku wako na vile unawahidumia.

3. Chumba cha kupanga(nyumba ambayo haijajengwa mahsusi kuwa Banda) sioni Kama itawafaa Sana maana kuku pia wanahitaji mwanga wa kutosha na hewa Safi inayoingia na kutoka. Kinyume na hapo usitegemee kupata matokeo mazuri.

Cha msingi jipange kununua chakula kiwepo cha kuwalisha kwa miezi hiyo 5, madawa, chanjo, mfanyakazi(Kama hautokuwepo mwenyewe) na nishati(umeme, mkaa au gas).

All the best ndugu, mungu akuongoze ukafanikiwe katika hilo.
 
Shukuran Mkuu nitalifanyia Kaz hili[emoji120][emoji120]
 
Sijajua mahesabu yako yapoje ila kuku 300 hupati tray 18 kwa siku umepata mengi ni 8 na si 18,kuku wa mayai wanahitaji pesa maana kama huna formula ya chakula chao basi itabidi ununue cha dukani maana wale si kama chotara utasema uwatupie pumba siku ipite,banda linatakiwa kuwa na hewa,banda liwe safi na kavu.jaribu kusoma vitabu au youtube uone jinsi ya kuvilea vifaranga maana chanagamoto nyingi ni week 6 za mwanzo,all the best
 
Hongera kwa kuwa na wazo kama ilo

Zingatia ya fuatayo

✓ Unataka kuku kutoka wazalishaji wapi. Maana kunawazalishaji wengi wa kuku wa mayai apa Tz kama vile Silver land, Interchick na n.k na kila mzalishaji kuku wake wanasifa Moja au Zaid inayotofautiana na mwingine kwanzia kwenye umli wa kutaga, kuvumilia magonjwa, idadi ya mayai kuku anayo taga kwa mwaka ( apa siwezi kuweka ni wazalishaji gani wazuri ivyo inabid uchunguze mwenyewe Mkuu maana izi ni biashara za watu)

✓ usafi wa vyombo vya maji
Jitaid uwe unaosha angalau kwa week mala mbili Mkuu kwa kutumia dodoki au steel wire ili kuepuka vifo maana ikitokea Kuna utelezi ndani ya vyombo vya maji basi apo ata uwape dawa gani sio lahisi kupona

✓ chakula
Apana unaweza kununua chakula kutoka kwenye maduka ya kuuzia vyakula vya mifugo au ukatengeneza mwenyewe kama ukitaka formular nitakupa buree kabisa Mkuu kwanzia stater hadi finisher

La mwisho ingawa sio lazima jitaidi kuku wakianza kutaga Yale mayai ya kwanza kabisa ata kama ni 30 mpelekee mchungaji au shekhee au mtu yoyote mwenye uhitaji apo utapata baraka kwa wingi na mayai yatakuwepo ya kutosha.
 
Shukuran mkuu nitakutafuta nikishaweka mipango sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…