Msaada kuhusu ufugaji wa kuku.

Chiwolanike

New Member
Joined
May 26, 2019
Posts
2
Reaction score
2
Habari wanajamvi?

Mimi ni Raia mpya jamvini na nimelazimika kuja huku ili nipate msaada wa ushauri juu ya changamoto niliyonayo.Nianze kwa kueleza nimekuwa kwenye ajira kwa vipindi vinne tofauti ingawa kwa zaidi ya miaka 7

lakini hakuna tija niliyopata kutokana na ajira hizo imefika wakati naona napoteza muda,hivyo nimekuja na wazo la ujasiliamali kupitia ufugaji wa Kuku.Wazo langu ni kufuga Kuku wa kienyeji kwa mtazamo wa kibiashara ingawa sijui lolote juu ya ufugaji wa kuku

.Ninao mtaji wa milioni 5 sina banda na naishi Geita kwenye nyumba ya kupanga.naomba mwongozo wenu kujua yafuatayo

1Ni aina gani ya kuku wa kienyeji wenye tija kibiashara.
2.Ni idadi gani yafaa kuanza nayo ili tija ionekane.
3.Ni banda la ukubwa gani litatosha kwa idadi hiyo.
4.Ni muda gani kuku anachukua toka kutotolewa mpaka kufaa kuliwa/kutaga.
5.Ni aina gani ya vyakula ambavyo vinaweza kufanya Kuku wakue vizuri.

Na mwisho niwaombe nisiwafunge na mawazo yangu mnishauri kadri mtakavyoona inafaa kwani hii sasa ni fainali.
 

Wataalam mjuzemi mdau
 
Jiunge na ma group ya ufugaji utajifunza mengi kabla ya kuanza mladi wako
 
Nitafute kwa namba 0752364906, nikupe na nikusaidie kufuga kitaalamu nimesomea fani ya mifugo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…