MSAADA KUHUSU UNUNUZI WA GARI LA SERIKALI LENYE NAMBA DFPA

Nundaaaatz

Senior Member
Joined
Oct 8, 2012
Posts
132
Reaction score
89
WADAU HABARI ZENU,
KUNA HALMASHAURI MOJA KWENYE BAJETI YA 2015/2016 IMEELEZA KUWA IMENUNUA GARI JIPYA KWA THAMANI YA MILIONI TISINI LAKINI CHA KUSHANGAZA GARI HIYO IMEKUJA NA NAMBA ZA USAJILI DFPA . KWA HIYO MADIWANI WAKAAMBIWA KUWA GARI HIYO IMENUNULIWA MPYA NA HALMASHAURI IPO KWENYE UTARATIBU WA KUBADILI NAMBA ILI KUPATA NAMBA SM.
JAMANI KWELI JAMBO HILI LIPO SAWA KULINGANA NA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA NA SHERIA NYINGINE ZA NCHI HII TANZANIA?
 
Taja hiyo halmashauri ili watu tuingie kazini
 
Kuna namna hapo sio bure.hiyo ni gari ya wafadhili/mradi ya halmashauri ingeanza na SM!
 
Kuna namna hapo sio bure.hiyo ni gari ya wafadhili/mradi ya halmashauri ingeanza na SM!
Ndio maana nikaomba msaada maana nikijua hilo ntawajulisha wahusika ili hela hiyo milion tisini irudi na wahusika washtakiwe!
 
Kuna uwezekano halmashauri imenunua hilo gari used toka kwa mashirika ya kimataifa likiwa ktk hali nzuri tu kwa lengo la kubana Matumizi. Sioni tatizo lipo wapi
 
Kuna uwezekano halmashauri imenunua hilo gari used toka kwa mashirika ya kimataifa likiwa ktk hali nzuri tu kwa lengo la kubana Matumizi. Sioni tatizo lipo wapi
SHERIA YA MANUNUZI INARUHUSU SERIKALI KUNUNUA MAGARI USED?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…