hakuna kitu kama hicho sheria za mirathi zinawatambua watoto,mke/wake/mume,baba na mama inategemeana na dini pamoja na mila za mlengwa lakini msimamizi wa mirathi kazi yake ni kugawa mirathi alivyoelekezwa kwa walengwa na hana fungu ktk mirathi na wala hakuna sheria ya namna hiyo isipokuwa kama yuko ktk kundi mojawapo ya niliyoyataja hapo juu.
lakini baada ya Mirathi kutoka anadai kuwa kisheria Msimamizi wa mirathi inatakiwa apewe Thelusi moja ya thamani yote ya mirathi.
Je ni sahihi kisheria?
Mkuu, ipo kisheria.
Hapa mkuu, inamaana kuwa mirathi imefuata sheria ya Mirathi au sheria ya kidini. Kwa maana kama utafuata sheria ya Dini Inamaana kua itabidi kufuata utaratibu kama Dini inavyoelekeza na hata mgawanyo lazima ufanyike ktk taasisi maalum kwa mujibu wa imani, sasa kwa upande wangu mimi nilipenda kujua kupitia Sheria yenyewe ya mirathi, je kuna kipengele kinachotaja haki halisi ya Msimamizi wa mirathi ktk Mirathi aliyosimamia? Sifahamu sheria hivyo kama nimekosea unaweza kunielekeza zaidi.Wakuu hata kidini, kimila nako ni "kisheria!" Mmesahau mambo ya Islamic Law, Customary Law, nk? Au neno "kisheria" lina maana gani kwenu?
download cover hapa chiniHapa mkuu, inamaana kuwa mirathi imefuata sheria ya Mirathi au sheria ya kidini. Kwa maana kama utafuata sheria ya Dini Inamaana kua itabidi kufuata utaratibu kama Dini inavyoelekeza na hata mgawanyo lazima ufanyike ktk taasisi maalum kwa mujibu wa imani, sasa kwa upande wangu mimi nilipenda kujua kupitia Sheria yenyewe ya mirathi, je kuna kipengele kinachotaja haki halisi ya Msimamizi wa mirathi ktk Mirathi aliyosimamia? Sifahamu sheria hivyo kama nimekosea unaweza kunielekeza zaidi.
Kama mirathi ilishatoka ina maana beneficiaries walishalipwa cheki zao (maana siku hizi kila mtu anapewa chake), sasa hilo suala la theluthi moja (1/3) linatoka wapi?
Sawa kabisa kama ulivyo eleza hapo juu, ila msimamizi wa Mirathi yeye sio beneficiar ktk hiyo mirathi. Je ni kweli anatakiwa alipwe na beneficiary hiyo thelusi aliyosema? ndilo swali langu.
Kifupi: Hakuna Sheria inayoeleza kwamba Msimamizi wa Mirathi anatakiwa alipwe theluthi (1/3) ya mirathi hiyo.
Hata hivyo, kama kuna gharama alizotumia Msimamizi, km usafiri, mazishi, nk anatakiwa arudishiwe!
Ndugu zangu naombeni msaada wa sheria inayohusu haki ya msimamizi wa mirathi baada ya mirathi kutoka.
Mama yangu alipata mtu ambaye alijitolea kua msimamizi wa mirathi, lakini baada ya Mirathi kutoka anadai kuwa kisheria Msimamizi wa mirathi inatakiwa apewe Thelusi moja ya thamani yote ya mirathi.
Je ni sahihi kisheria? Ni hayo tu ndugu zangu.
Asante sana Mh. assuredly4 maelezo yako pia nimeyaelewa vizuri sana. Kwakua gharama zote za kufuatilia pamoja na mahitaji yote muhimu pamoja na posho za kufuatilia tulilipa wenyewe, tupo ktk hatua za kumuondoa ktk usimamizi kabla B.O.T hawajatulipa hili kuepuka visasi na migogoro isiyo na sababu si unajua tena wengine huwa wanawaza kudhulumu tu.