Inawezekana. Ila kwa kweli ni vigumu kukuelezea maana sina majibu ya maswali mengi muhimu juu ya mtiririko wa ugonjwa aliokuwa nao mgonjwa na dalili zake.
Kwa mfano tu, kati ya kazi ya ini ni kutengeneza aina fulani ya protein inayoitwa "albumin" ambayo husaidia damu na maji kukaa katika mishipa ya damu na kuboresha mzunguko wa damu na virutubisho sehemu mbalimbali za mwili ikiwa ni pamoja na figo. Sasa mtu anaweza akawa na tatizo la ini, tatizo hilo likasababisha upungufu wa albumin, maji yakapungua toka katika mishipa ya damu, ikasababisha upungufu wa mzunguko wa damu sehemu mbalimbali za mwili ikiwa ni pamoja na figo, na mtu akapata tatizo la figo (renal failure).
Huo hapo juu ni mfano mdogo tu, na hauna maana ya kwamba hilo ni tatizo alilokuwa nalo mgonjwa. Kwa kweli ningependa kusaidia wadau hapa kuelewa hili, lakini kwa maelezo uliyotoa hayajitoshelezi na nisingependa kukisia tu maana matatizo yanayoweza kusababisha hilo yapo mengi.
Nimetumia mfano huo hapo juu kwa ajili tu ya kuonyesha uhusiano unaoweza kuwepo kati ya viungo hivi viwili na sina maana kwamba hilo ndiyo tatizo alilo nalo mgonjwa. Naomba nieleweke hivyo.