Msaada Kuhusu Vidonge Vya Uzazi Wampango(vidonge Vya Familia)

Kanizi

Member
Joined
Nov 30, 2014
Posts
38
Reaction score
6
Kuna rafiki Yangu Ameshauliwa Na Dk Atumie Vidonge Hivi Ili Kuregurate Homon Zake Baada Ya Kutoziona Siku Zake Kwa Kipindi Cha Miezi 2 Na Wiki 2 Baada Ya Kujifungua. Je Vidonge Hivi Vina Weza Kuwa Na Madhara Yoyote Apo Baadae Kwake Au Kwa Mtoto Iwapo Atajaliwa Kumpata? Kama Yapo Ni Yapi? Msaada Tafadhar.
 
Nadhani ni vyema angefanya vipimo kubaini kama ameshika tena ujauzito au la. Vinginevyo sidhani kama ni salama kula hivyo vidonge ilihali akiwa ni mjamzito. Akiwa hana ujauzito basi anaweza kutumia vidonge vile vinavyosaidia kutoshika ujauzito mpaka hapo atakapokuwa teyari! Ngoja tusubiri wenye kufahamu madhara ya hivi vidonge watupe elimu.
 
Kuna mambo ya kuzingatia.

1. Je kunyonyesha? Kama ananyonyesha, kutokupata siku sio jambo la kushangaza.

2. Iwapo ameamua kutumia ni muhimu kujua aina gani ya kutumia. Zipo dawa nyingine zinapunguza maziwa na anaweza kujikuta anakosa cha kumnyonyesha mtoto.

Pata majibu ya mambo hayo mawili halafu njoo kwa ushauri zaidi...
 

Apana Anyonyeshi Kwan Wakati Wa Kujifungua Mtoto Alifia 2mboni. Na Vidonge Alivyopewa Vinaitwa Vidonge Vya Familia.
 
Apana Anyonyeshi Kwan Wakati Wa Kujifungua Mtoto Alifia 2mboni. Na Vidonge Alivyopewa Vinaitwa Vidonge Vya Familia.

Kama hanyonyeshi anaweza kutumia vidonge hivyo.
In general hakuna dawa isiyo na madhara, kwahiyo siwezi kukupa jibu la asilimia 100 kuwa havitamdhuru ila daktari wake atakuwa ameangalia historia yake na kujua kuwa vinamfaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…