Msaada kuhusu vyuo vya Jordan University Colloge na SAUT-Arusha Campus

humility21

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2021
Posts
448
Reaction score
622
Ndugu zangu nina mdogo wangu amefanikiwa kuchaguliwa ktk vyuo hivi viwili vya elimu ya juu vya Jordan University College kilichoko Morogoro na St. Augustine University - Arusha Campus. Naomba mwenye kuvijua vyuo hivi vizuri kwenye upande wa miundo mbinu, mazingira na ubora wa elimu anisaidie kunipa taarifa. Natanguliza shukrani kwenu.
 
Huyo mdogo wako ni freshers kwa maana ametoka form six au ni inservice na kachaguliw coz ipi?
 
Mmmh Chuo ni chuo lakin mbna kama alikurupuka ?
 
Aende Jordan ni chuo cha zamani sema kilikuwa ni maalumu Kwa degree ya philosophy na Theology Kwa ajili ya mapadre wa kikatoliki, binafsi nilisoma philosophy hapo kabla wito haujanishinda.
Hiyo campus ya Arusha ni mpya mpya changamoto Zitakuwa nyingi
 
Aende jordan morro ....campus ya arusha iko town kati na sio kubwa sana ina changamoto nyingi
 
nipo jordani hapa mwaka wa pili karibu sana (mimi ni mdada)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…