Msaada: Kuna sheria ngapi za mirathi?

Mchokoo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
1,181
Reaction score
1,579
Kuna sheria za mirathi aina ngapi hapa nchini?

Je, wa kike anaruhisiwa kurithi ardhi sawasawa na wa kiume?
 
Kuna sheria za mirathi aina ngapi hapa nchini?
Je, wa kike anaruhisiwa kurithi ardhi sawasawa na wa kiume?
1.Zipo Sheria za Mirathi za aina mbalimbali hapa Tz,, muone Wakili ili akusaidie ktk hili.

2.Endapo kama hakuna wosia au vikwazo vingine vyovyote vile vya kisheria, Makundi ya Warithi halali wa Mali za marehemu wanaotambulika kisheria ni hawa wafuatao:-

1) Mwenza au Wenza wa Marehemu.
2) Watoto wa Marehemu.
3)Wazazi wa Marehemu.

NOTE:- Kwenye makundi yote hapa juu, Sheria haijaainisha Jinsia ya Mrithi.

Aidha, watajwa hapa juu ni kundi la Kwanza kabisa la watu ambao Wana haki ya moja kwa moja ya kurithi mali za marehemu. Kuhusu makundi mengine ya warithi wengine endapo kama watajwa wote wa hapo juu hawapo, pata ushauri wa Wakili aliye karibu nawe.
 
Je WATOTO ni wale wa NDOA au hata wa NJE ya NDOA?
 
Je WATOTO ni wale wa NDOA au hata wa NJE ya NDOA?
Watoto wote Wana haki sawa, iwe wa nje ya Ndoa au ndani ya Ndoa,tena unaweza kuta hao Watoto wa Ndoa Baba kapigwa na ukakuta wale wa nje ya Ndoa ndiyo copy right na baba!! Jitafakari Mtoto ni Mtoto tu!!
 
Je WATOTO ni wale wa NDOA au hata wa NJE ya NDOA?
Ili kujua ukweli kua Mtoto gani anatakiwa kurithi, inatakiwa Watoto wote wakapime DNA,mkisha pata majibu ya DNA hapo ndiyo mtajua wa ndani nani na wa nje Nani!!
 
Je WATOTO ni wale wa NDOA au hata wa NJE ya NDOA?
Watoto wote halali wanaotambulika ambao wameachwa na marehemu, wakiwamo watoto wa ndoa, watoto wa nje ya ndoa ambao wanatambulika na wanandugu au warithi wengine, pamoja na watoto wengine walioasiliwa kisheria na marehemu enzi za uhai wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…