Msaada: Kuna ukweli hapa wataalamu?

Mirhea

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
814
Reaction score
1,382
Kuna ndugu yangu kanitumia hizi screenshots bila maaelezo ya ziada.
Nimejaribu kutafuta kwenye media husika pasipo mafanikio.
Ila naamini hapa sitatoka kapa.

Natanguliza shukrani
 
Nimekuwekea link ya habari hapo juu,ila kwa kifupi ti si kwamba keyless ndo zinasababisha au zinatoa carbon monoxide kuliko zile zenye kutumia ufungio. Tatizo ni kwamba watu huwa wanasahau na kuacha ingine idling kwenye closed garage. Hapo ndo issue ya carbon monoxide inapotokea sasa. Hata zile gari za kuwasha na funguo ukiacha idling kwenye closed garage zinatoa carbon monoxide vile vile. Asante
 

Watu kama nyie ndio tunawahitaji hapa. Karibu sana.
 
sijaelewa bado chief!

ukiacha idling kwenye closed garage kivipi?
 
sijaelewa bado chief!

ukiacha idling kwenye closed garage kivipi?
Mkuu samahani kama nimekuchanganya,kwa huku nilipo neno garage ni sehemu unayopaki gari au kuhifadhi hardware kadhaa nyumbani kwako.Kuna zile ambazo zipo wazi na kuna zile ambazo zipo closed na mara nyingi huwa zimeunganishwa na nyumba.Yaani ukiingia garage kupaki gari mlango wa garage unafungwa wewe unaingia ndani ya nyumba( Unaweza ku type closed garage kwenye google kisha ukaona images ndo utanielewa vizuri). Sasa hapo issue ni kwamba unapoacha gari inaunguruma hata kwa dakika 5 tu kisha ukarudi ndo shughuli ya carbon monoxide utakapoifahamu.Nafikiri umenielewa kiongozi.
 
sasa nimekuelewa, asante sana.

kwahiyo tatizo hapo sio gari ila ni eneo ambalo umeweka gari? kwamaana navyoelewa mimi kila gari inaEmit carbonmonoxide.
 
Sorry again. Vipi kuhusu mapungufu ya Touareg ni toleo lipi haswa 2010 au 2016?
Je kwani wazirecall tuu hizo za China na sio worldwide?
Zilizopo huku Bongo hilo tatizo hazina?
 
sasa nimekuelewa, asante sana.

kwahiyo tatizo hapo sio gari ila ni eneo ambalo umeweka gari? kwamaana navyoelewa mimi kila gari inaEmit carbonmonoxide.
Upo sawa kabisa hapo kiongozi.
 
Sorry again. Vipi kuhusu mapungufu ya Touareg ni toleo lipi haswa 2010 au 2016?
Je kwani wazirecall tuu hizo za China na sio worldwide?
Zilizopo huku Bongo hilo tatizo hazina?
Kwanza kabisa naomba nikuambie kuwa kwenye magari,recall huwa ni jambo la kawaida sana na linatokea mara kwa mara. Kama upo Tanzania ni vigumu sana kujua kuhusu recall kwa kuwa magari tunayonunua huko huwa ni ya muda mrefu sana.Kama ukigoogle any car make kwa mfano uweke BMW au marcedes recall utaona models zilizokuwa recalled,au kama unakumbuka Takata airbag recall kama miaka mitatu iliyopita.
Haya narudi kwenye topic ya Toureg,kwanza naomba uelewe kuwa kwa sheria za uwekezaji za China,lazima foreign car manufacturer awe na joint venture na kampuni ya kichina,inawezekana nipo wrong lakini ndo ninavyokumbuka hivyo. Kwa hiyo recalls ni kwa hizo Tourage zilizotengenezwa China kwa miaka hiyo. Zinazoingia Tanzania sidhani kama zina recall maana huwa zinatokea German/Japan/South africa atc atc.
Nafikiri nimekujibu.
 
Sorry again. Vipi kuhusu mapungufu ya Touareg ni toleo lipi haswa 2010 au 2016?
Je kwani wazirecall tuu hizo za China na sio worldwide?
Zilizopo huku Bongo hilo tatizo hazina?
Za bongo mshachafua sana seat mnapigia show kwenye gari. Nyie endesheni hivo hivo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…