Ndugu wadau nimekuwa nikifuatilia Bunge kwa umakini sana na Kuona Chama cha demokrasia na Maendelea CDM wakitoka nje kwa kukataa kuendelea kujadili muswada wa Mapendekezo ya Katiba mya kwa kutaka usomwe kwa mara ya Kwanza.. wakimaanisha uli ulio somwa kwa mara ya kwanzqa ulikataliwa na wabunge wote kwasababu uliandikwa kwa Lugha ya Kiingereza kwa maana hiyo ni Zero. kama wameanza upya.
Bado sijajua Faida zake je Munaweza niaidia ili namimi nikiona wanatoka nijue labda wanania ya Kutusaidia sisi Watanzania au wanania ya kuuchelewesha uhondo wa katiba itakayo tusaidia sisi wananchi wa chini? nitafurahi sana kupata details za kutosha
Kwa mujibu wa katiba hii iliyopo:
A proposal for a new law i.e BILL should be read twice before the house of representatives. Kusomwa kwa mara ya kwanza ni kuruhusu amendments toka kwa wabunge na wadau wengine. Baada ya kusomwa huku, yale mapendekezo hurudishwa ktk CABINET kufanyiwa marekebisho ikiwa Rais (Head of the Cabinet) ataona mapendekezo hayo yanafaa. Baada ya maboresho (au bila maboresho) muswada huo utarejeshwa kwa mara ya pili kuangaliwa vipengele vilivyofanyiwa marekebisho ili kuruhusu more amendments. Na baadae tena mswada unarudishwa kwa Rais na baraza la mawaziri wataangalia tena mapendekezo ya wabunge. Kama wabunge wameukubali, Rais atausaini na tangu hapo mswaada huo unakuwa SHERIA. Na ikiwa wabunge wameugomea kwa mara ya pili, Rais analazimika kulivunja bunge.
ISHU YA KATIBA: Muswada wa uundwaji wa tume ya kuratibu uandikwaji wa katiba mpya ulipelekwa bungeni kwa lengo la kusomwa mara ya kwanza. Kweli ulisomwa, lkn ulikataliwa na wabunge wote kwa ujumla wao kwa sababu kuwa na mapungufu makubwa yaliyosababisha hata usijadilike. Kengo lilikuwa uandikwe upya kwa misingi yenye kujadilika. Serikali ikaurejea na kuuandika upya kwa kiswahili na ndio juzi hapa wameupeleka tena bungeni. Mzozo uliopo ni serikali kuusoma kwa mara ya pili, badala ya mara ya kwanza. (ukumbuke mswada husomwa mara ya kwanza kuruhusu amendments, sasa huu haukufanyiwa amendments bali structure yake ndio iliyokosolewa). Wanachodai CHADEMA na wanaharakati ni kwamba, taratibu za msingi za kuunda tume ya kuratibu uchukuaji maoni, ndio msingi wa ufanisi wa shughuli yenyewe na hii ni kweli kabisa. Sasa kama jambo hili litafanywa kwa makosa, hata maoni yatakayotolewa hayatakuwa na faida sanasana yataishia mikononi mwa Rais ambaye amepewa mamlaka ya kuamua nini afanyie maoni hayo.
Kwa mtazamo wa haraka haraka wa katiba ya zamani, madaraka makubwa aliyonayo rais ndio tatizo la maendeleo ya nchi yetu. Sasa hofu ya wanaharakati (na watanzania wote wenye kuelewa nini kinaendelea) ni kwamba hata uundwaji tu wa tume ya kuratibu upatikanaji wa katiba mpya tayari unahodhiwa na serikali badala ya wananchi.
Kwa hiyo summary ya huu mzozo ni kwamba, muswada ule unasomwaje kwa mara ya pili ikiwa haukusomwa mara ya kwanza?
Ukilitafakari hili utagundua kuwa CCM bado hawana nia ya dhati ya kuona uwajibikaji unakuwa sehemu ya utamaduni wetu. Na ndio maana hawako tayari kuona tuna mamlaka ya kumwajibisha kiongozi