Msaada: Kuna uwezekano wa kufanyia interview katika kituo kilichopo katika mkoa niliopo sasa?

thee kid

Member
Joined
May 13, 2019
Posts
66
Reaction score
50
Habari ndugu zangu?

Natumaini mko salama na wazima wa afya.

Samahani naomba kuuliza jambo ninechaguliwa katika online written interview za utumishi lakini kituo nilichopangiwa ni mkoa mwingine mbali kabisa na mkoa niliopo sasa ivi.

Nilikuwa nauliza kama kuna uwezekano wa kufanyia interview hii katika kituo kilichopo katika mkoa niliopo sasa ivi?
 
Soma Tangazo la juzi vyema. Wamesema Kila msailiwa atafanyia katika mkoa wa makazi alioonesha Kwenye Taarifa binafsi za NIDA. Lakini pia muda Bado ni mrefu mambo mengi yananafasi ya kurekebishwa. Maana unatakiwa kufanyia mkoa wa makazi yako ya sasa.

KNY. Tangazo.😊
 
Nazan abadl taharfa ktk taharfa zake mahal anapoish aweke za sasa kqbla labda tarehe 6
 
Inawezekana kabisa mkuu wala usiangaike kutumia nauli! Kikubwa kada iwe moja! Kwa sababu lengo la wao kuweka mikoa ni kuwapunguzia gharama! Kikubwa wasiliana nao wakubadilishie! Na hata usipowapata siku ile ya interview wahi eneo la tukio waambie snario yako! Wala hakuna shida kabisa! Kuna mtu alipangiwa ruvuma lakini siku ya usaili alifanyia mtwara! System zinasomana hakuna kitachoharibika
 
Thanks sana mkuu nilifanikiwa
 
Naombeni hiyo list ya majina wakuu, me niliomba Tax Management Assistant II. Kuna list nimeiona ila hiyo Tax Management Assistant II haipo kabisa.
 
Inawezekana, wasiliana nao mapema . Ukishindwa kuwapata, siku ya usahili wahi kwenye kituo cha usahili uwaanbie watasiliana wenyewe kwa wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…