Kwanza,kama hutajali,ningenda utujibu swali hili:
Ikiwa umesema ni kawaida yako kupitiliza siku,ni kwanini leo una hofu kwa kupitiliza mwezi uliopita?
Kusema kweli hakuna mtu mwenye jibu sahihi kwa jambo hili kwa muda huu.
Kwa nini?
Kwanza,umesema siku zako hazieleweki,kwa maana kwamba kuna wakati unapitiliza.Kwa hiyo kama mwezi uliopita hujaziona huenda ikawa ni kama miezi mingine unayopitiliza na kwa maana hiyo hujashika mimba!
Pili,kuna wanawake wengine wanaweza kushika mimba na bado wakaendelea kuona siku zao(japo sio kawaida) kwa mwezi unaofuata na hata wa pili. Kwa hiyo,kuona siku zako hakiwezi kuwa kipimo cha kwamba hujashika mimba dada!
Nini cha kufanya?
Kwanza,angalia utatumia siku ngapi.Ikiwa utatumia siku ulizozoea(3,4,5,7 nk) kama zitakuwa zile zile unaweza kufikiria pengine hujashika mimba..ingawa jibu sahihi ni kufanya vipimo hapo baadaye kidogo.
Nahisi ni kama hujajiandaa kubeba mimba kwa muda huu,na pengine ndipo hofu yako inapotokea,au nakosea?Kama ndivyo,ili kujiweka huru,unaonaje kama mngekaa na mwenzio mkashauriana na pengine kutafuta njia sahihi itakayowafaa ya kuzuia kushika mimba..I mean family planning?
Na kuhusu swali lako kwamba nini tatizo hapo,ni kwamba,binadamu tunatofautiana kimaumbile.Vitabu vinaandika juu ya maumbile,mabadiliko na mwenendo wa maisha ya binadamu.Wanapoandika na kutufundisha kuwa mwanamke ataona siku zake kila mwezi,wamefanya utafiti kisha wakageneralize kutokana na wanawake wengi kufanana.Ila hiyo haiondoi ukweli kwamba kuna wachache ambao kimaumbile wana mienendo tofauti na hawana shida yoyote..kwa maana kwamba wao ndivyo walivyo na ndio kawaida yao.
Range ya kawaida ya mzunguko wa siku ni kuanzia siku 21 hadi 35.Kwa maana kwamba kuna wanawake ambao wao mzunguko wao ni siku 21 tu ilhali wengine hufika hadi siku 35! Kutokana na wanawake wengi mzunguko wao kuwa ndani ya mwezi mmoja,ndipo wakatafuta wastani wa 21 na 35 wakapata 28! Sasa kwa vile watu wengi tumekariri hiyo 28 ndio maana mtu akipitasha siku hizo anajihesabu kama amepitiliza mwezi,lakini kiukweli anakuwa bado yupo kwenye range ya kawaida(21 - 35).
Of course yapo mengi ya kueleza..ila kwa leo naomba niishie hapa kwanza.