Msaada: Kuna uwezekano wa kupata mimba leo?

mchoyo

Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
48
Reaction score
8
habar zenu,polen na majukumu mimi Ninaish na mume wangu huwa na kawaida ya kupitiliza cku, sasa mwez uliopita nilipitiliza mwez mzima,sasa leo saa kumi na mbili tulikutana kimwili imefika mda huu zimeanza nn tatizo hapo?na kuna uwezekano wa kupata mimba leo?
 
mi naona kama nimeeleweka kipi labda cjakieleza vzr nambie nikuweke sawa
 
sory topic imejirudia maneno ya chini hapo nilioyaandika
 
Kwanza,kama hutajali,ningenda utujibu swali hili:
Ikiwa umesema ni kawaida yako kupitiliza siku,ni kwanini leo una hofu kwa kupitiliza mwezi uliopita?

Kusema kweli hakuna mtu mwenye jibu sahihi kwa jambo hili kwa muda huu.

Kwa nini?

Kwanza,umesema siku zako hazieleweki,kwa maana kwamba kuna wakati unapitiliza.Kwa hiyo kama mwezi uliopita hujaziona huenda ikawa ni kama miezi mingine unayopitiliza na kwa maana hiyo hujashika mimba!

Pili,kuna wanawake wengine wanaweza kushika mimba na bado wakaendelea kuona siku zao(japo sio kawaida) kwa mwezi unaofuata na hata wa pili. Kwa hiyo,kuona siku zako hakiwezi kuwa kipimo cha kwamba hujashika mimba dada!

Nini cha kufanya?

Kwanza,angalia utatumia siku ngapi.Ikiwa utatumia siku ulizozoea(3,4,5,7 nk) kama zitakuwa zile zile unaweza kufikiria pengine hujashika mimba..ingawa jibu sahihi ni kufanya vipimo hapo baadaye kidogo.

Nahisi ni kama hujajiandaa kubeba mimba kwa muda huu,na pengine ndipo hofu yako inapotokea,au nakosea?Kama ndivyo,ili kujiweka huru,unaonaje kama mngekaa na mwenzio mkashauriana na pengine kutafuta njia sahihi itakayowafaa ya kuzuia kushika mimba..I mean family planning?

Na kuhusu swali lako kwamba nini tatizo hapo,ni kwamba,binadamu tunatofautiana kimaumbile.Vitabu vinaandika juu ya maumbile,mabadiliko na mwenendo wa maisha ya binadamu.Wanapoandika na kutufundisha kuwa mwanamke ataona siku zake kila mwezi,wamefanya utafiti kisha wakageneralize kutokana na wanawake wengi kufanana.Ila hiyo haiondoi ukweli kwamba kuna wachache ambao kimaumbile wana mienendo tofauti na hawana shida yoyote..kwa maana kwamba wao ndivyo walivyo na ndio kawaida yao.

Range ya kawaida ya mzunguko wa siku ni kuanzia siku 21 hadi 35.Kwa maana kwamba kuna wanawake ambao wao mzunguko wao ni siku 21 tu ilhali wengine hufika hadi siku 35! Kutokana na wanawake wengi mzunguko wao kuwa ndani ya mwezi mmoja,ndipo wakatafuta wastani wa 21 na 35 wakapata 28! Sasa kwa vile watu wengi tumekariri hiyo 28 ndio maana mtu akipitasha siku hizo anajihesabu kama amepitiliza mwezi,lakini kiukweli anakuwa bado yupo kwenye range ya kawaida(21 - 35).

Of course yapo mengi ya kueleza..ila kwa leo naomba niishie hapa kwanza.
 
kaka sio kama cpo tayar kubeba nipo tayar mda wowote ule coz naish nae pamoja i mean wanandoa tayar kinachonisumbua ni huu mzunguko unavyo badilika kama kinyonga adi nakosa raha
 
Kama paragraphs mbili za mwisho hujaridhika nazo,unaweza kusema..ili nijaribu kutoa maelezo kwa upande wa pili.
 
mi naona kama nimeeleweka kipi labda cjakieleza vzr nambie nikuweke sawa
Huwezi kupata mimba kama zimeanza jioni ya leo make mda wa matarajio kupata mimba ni kuanzia siku ya nane hadi ya kumi na nne.
 
Huwezi kupata mimba kama zimeanza jioni ya leo make mda wa matarajio kupata mimba ni kuanzia siku ya nane hadi ya kumi na nne.

Na hapa ndipo tunapokosea sana.

Ni vema tukatambua kwanza kwamba,kuonekana kwa bleed,maana yake ni kwamba muda ambao mimba ilitakiwa kutunga haikufanikiwa,ndio maana baada ya siku kadhaa kupita,ukuta wa mji wa uzazi uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya kupokea hicho kiumbe,unabomoka ili mzunguko mwingine uanze.Kwa mantiki hiyo ni kwamba,tulitakiwa kuhesabu hivyo kuanzia siku ya kwanza alipoanza kuona siku zake za mwisho kabla ya hii ya sasa.

Na ni vema pia ikaeleweka kwamba,haya mahesabu ya kalenda yanakuwa na maana tu ikiwa siku za huyu dada hazibadiliki hata kidogo.Lakini hayana maana yoyote ikiwa periods zake ni irregular kama ilivyo kwa huyu dada yetu.Na hili jambo watu wamekuwa wakilichukulia kijuu juu sana,na matokeo yake,wengine wamekuwa wakilaumiana sana na hata wakati mwingine wanaume wanakataa mimba ambazo kiukweli ni zao kabisa!

Hesabu hizi zina maana pia ikiwa mzunguko wa mwezi ni siku 28,lakini hayana maana yoyote ikiwa mzunguko ni wa siku 21-25 au 31-35.Kwa hiyo ni vema watu waelewe jambo hili vizuri jamani.Na hata kama ni mzunguko wa 28 days,matarajio siku ya 14 lakini inaweza kuwa siku mbili kabla au siku 2 baada ya 14,kwa lugha yepesi, ni kati ta siku ya 10-16. Kwa hiyo kwa hii hesabu yako inaweza kuwa na maana tu ikiwa mzunguko utakuwa wa chini ya siku 26. But kama ni mzunguko wa siku 28(za kawaida),mwanaume ataikataa mimba mchana kweupeee.. Maana siku ya 14,15 na 16 bado ni siku hatari!

Lakini nasisitiza jamani,binadamu sio kitabu.Tunatofautiana. Kwa hiyo na hii habari ya kalenda inatofautiana pia kimahesabu kati ya mwanamke mmoja na mwingine.
 
ni kweli wanawake tunatofautiana kama mm ndo cjielew kabisa coz mwez wa nne niliingia date 23 mwezi wa tano date 23 kimbembe mwez wa sita cjaziona kabisa adi leo date 9 mwez huu nimeona hapo nnanisaidiaje kimawazo jaman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…