Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Wakuu kwema??
Ninalo shamba mahali ambako nilipanga nichimbe kisima kirefu kwa ajili ya Kuweka Drip Irrigations System ambako ningekitumia hicho Kisima. Sasa kuna Rafiki yangu mmoja yuko kama kilometer 1 hivi kutoka hapo kwangu alinitangulia kuchimba kisima chake kama miezi 6 hivi kabla yangu, Ye alichimba kwake na aliishia Mita 60 akawa anapata maji safi tu muda wote na hayakatiki.
Mimi kuja kuchimba changu sikufanya survey bali nilimwambia mchimbaji achimbe tu hizo hizo 60 kama za jamaa tuone, na tukapata maji kweli masafi na mengi tu tukaamua kuishia hapo na kuchimbia/kudumbukiza Bomba za Plastic (PVC).
Sasa shida imekuja, kumaliza wiki tu maji yamekata hakuna maji tena. Nimewaza nizichomoe zile Bomba ili niendelee kuchimba zaidi pengine mpaka mita 80 au hata 100. Wale walionichimbia mwanzo wamenishauri niingie tu Gharama kuchimba upya kingine kirefu zaidi kwani haiwezekani tena kuchomoa zile Bomba.
Sasa hapa naomba ushauri tu kwa wazoefu wa haya mambo, je ni kweli haiwezekani kuchomoa bomba? Au Altenatively naweza kufanya nini hapa? Karibuni