Msaada; Kuondoa Pipes Kwenye Kisima Kirefu

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Wakuu kwema??

Ninalo shamba mahali ambako nilipanga nichimbe kisima kirefu kwa ajili ya Kuweka Drip Irrigations System ambako ningekitumia hicho Kisima. Sasa kuna Rafiki yangu mmoja yuko kama kilometer 1 hivi kutoka hapo kwangu alinitangulia kuchimba kisima chake kama miezi 6 hivi kabla yangu, Ye alichimba kwake na aliishia Mita 60 akawa anapata maji safi tu muda wote na hayakatiki.

Mimi kuja kuchimba changu sikufanya survey bali nilimwambia mchimbaji achimbe tu hizo hizo 60 kama za jamaa tuone, na tukapata maji kweli masafi na mengi tu tukaamua kuishia hapo na kuchimbia/kudumbukiza Bomba za Plastic (PVC).

Sasa shida imekuja, kumaliza wiki tu maji yamekata hakuna maji tena. Nimewaza nizichomoe zile Bomba ili niendelee kuchimba zaidi pengine mpaka mita 80 au hata 100. Wale walionichimbia mwanzo wamenishauri niingie tu Gharama kuchimba upya kingine kirefu zaidi kwani haiwezekani tena kuchomoa zile Bomba.

Sasa hapa naomba ushauri tu kwa wazoefu wa haya mambo, je ni kweli haiwezekani kuchomoa bomba? Au Altenatively naweza kufanya nini hapa? Karibuni
 
Duh unazingua karibia bomba 20 Hivi za futi Ishirini?? Aiseeee Sidhani kama kuna namna ya kuzitoa, Usije kukubali kudanganywa maana hata ukifikiria tu Kwa hali ya kawaida ni ngumu.
 
Duh unazingua karibia bomba 20 Hivi za futi Ishirini?? Aiseeee Sidhani kama kuna namna ya kuzitoa, Usije kukubali kudanganywa maana hata ukifikiria tu Kwa hali ya kawaida ni ngumu.
Kuna mmoja amenishauri nikodi "Chain Hoist Crane" kiswahili chake sijui yaitwaje,
Kisha niizamishe mpaka chini kabisa ya Pipe (60 meters) down kisha ikinasa kwenye bomba la mwisho nianze kuvuta juu. Sielewi hii imekaaje yaani Mkuu,

Hasara yake hiki kisima na vyuma vilivyo dah
 
Unaweza kufanikiwa lakini uwezekano wa kupata bomba zote kamili ni mdogo unaweza kupata nusu au robo tatu ya hayo mabomba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kufanikiwa lakini uwezekano wa kupata bomba zote kamili ni mdogo unaweza kupata nusu au robo tatu ya hayo mabomba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa Pia Mkuu nawania kuokoa kuchimba mita zingine 80 mpya, so Bomba zikitoka zote hata kama zitatoka zimepasuka mradi kwenye kuchimba nitachimba mita 20 au 30 tu kama nikiendeleza shimo lile lile
 
Hapa Pia Mkuu nawania kuokoa kuchimba mita zingine 80 mpya, so Bomba zikitoka zote hata kama zitatoka zimepasuka mradi kwenye kuchimba nitachimba mita 20 au 30 tu kama nikiendeleza shimo lile lile
Kwani hao waliokuchimbia mwanzo wamekwambia ucimbe kipya kwa sababu gani? Je, umewaambia hilo wazo la kwamba hata zikipasuka kwako ni fresh tu wamesemaje?
 
Kwani hao waliokuchimbia mwanzo wamekwambia ucimbe kipya kwa sababu gani? Je, umewaambia hilo wazo la kwamba hata zikipasuka kwako ni fresh tu wamesemaje?
Wao ni Wafanyabiashara,
Nimewaza wanataka nichimbe kipya ili wachukue hela zaidi,
Kuhusu Bomba wamesema haziwezi kutoka hata kwa kupasuka
 
Habari mm ni mchimbaji wa visima kila maeneo yana water level yake hapo inaonekana alie chimba amefata maelezo yako ya mita 60 hakuangalia sample ya mwamba wenye maji katika uchimbaji kila baada ya mita 2 lazima upange sample ili ujue jinsi ya kupangilia bomba katika PVC kuna screen na plane sample ndy inaonesha jinsi ya kupanga PVC tena kwa mchoro jinsi sample zilivyo onesha. Hapo kuna mawili pengine bomba zimewekwa bila ya mpangilio wa sample au sio water level ya eneo husika ambayo imechibwa. Na PVC zikisha wekwa ukweli haziwezi kutoka. Hakuna sababu ya kukosa maji endapo mchimbaji atazingatia sample zitakavyo onesha hata angechimba mita 100 ila akikosea kupanga bomba hakuna maji. Kwa ushauri au mahitaji yoyote kuhusu huduma ya kisima tuwasiliane : 0688525288
/0653677815 kazi zetu ni za uhahika
 
Dah,
So mkuu wanishauri nini labda?
Maana kuchimba Upya tena from Zero hiyo hela kwa sasa sinayo yaani
 
tatizo wewe mwenyewe unjitia kujua, kwanini hukuwashirikisha mapema hao mafundi maji, badala yake wewe ndo uliagiza, chimna hapa, halafu mnamlaum Museveni hashauriki!
 
Mkuu Shark huu ushauri ni sahihi kabisa, niliwaona jamaa wanavyochimba! Uwezekano wa kuzitoa ni mdogo saana maana hazina viunganishi
 
Mkuu Shark huu ushauri ni sahihi kabisa, niliwaona jamaa wanavyochimba! Uwezekano wa kuzitoa ni mdogo saana maana hazina viunganishi
Mimi sikuwepo wakati wakitumbukiza hizi Pipes,
Lakini nilidhani kuna male-female connection kati yao, kama wanavyounga pipes za majumbani labda
 
Mimi sikuwepo wakati wakitumbukiza hizi Pipes,
Lakini nilidhani kuna male-female connection kati yao, kama wanavyounga pipes za majumbani labda
Mkuu kama haukuwepo pengine hakikufika mita ulizotaka ilitakiwa uwepo ujue bomba ngapi zimeingia kila bomba 1 ina mita 3 au jaribu kutafuta kitu ambacho unaweza kupima ili ujue kama kwel walitimiza hizo mita 60
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…