Hizo nyumba hazipangishwi kwa uwazi
Hizo nyumba wamepewa watu waliokuwa wanaishi nyumba za zamani zilizovunjwa. Wamepewa waishi bure bila kulipa kodi kwa miaka mitano.
Na wamekatazwa kabisa kupangisha maana wakigundulika wanaporwa mkataba.
Kwa ujanja uwa wanaziuza . Yaani anakuuzia haki yake ya kuishi pale kwa miaka mitano yote.. anakupigia hesabu ya kodi ya kila mwezi kwa miezi 60. Then unamlipa yote yeye anakuachia nyumba yake.. hawezi kukubali kodi ya miezi 6 sababu anajua ni kosa kubwa na ikigundulika ataporwa haki yake ya miezi yote 60
Kama unataka kuishi pale ni lazima umtafute mtu mwenye haki ya kuishi pale muongee akuuzie haki yake ya kuishi